1
Waefeso 6:12
Neno: Bibilia Takatifu
Kwa maana kushindana kwetu si juu ya nyama na damu, bali dhidi ya falme, mamlaka, dhidi ya wakuu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
Linganisha
Chunguza Waefeso 6:12
2
Waefeso 6:18
Mkiomba kwa Roho siku zote katika sala zote na maombi, mkikesha kila wakati mkiwaombea watakatifu wote.
Chunguza Waefeso 6:18
3
Waefeso 6:11
Vaeni silaha zote za Mungu ili kwamba mweze kuzipinga hila za ibilisi.
Chunguza Waefeso 6:11
4
Waefeso 6:13
Kwa hiyo vaeni silaha zote za Mungu ili mweze kushindana siku ya uovu itakapokuja nanyi mkiisha kufanya yote, simameni imara.
Chunguza Waefeso 6:13
5
Waefeso 6:16-17
Zaidi ya haya yote, twaeni ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. Vaeni chapeo ya wokovu na mchukue upanga wa Roho, ambao ni Neno la Mungu.
Chunguza Waefeso 6:16-17
6
Waefeso 6:14-15
Kwa hiyo simameni imara mkiwa mmejifunga kweli kiunoni na kuvaa dirii ya haki kifuani, nayo miguu yenu ifungiwe utayari tuupatao kwa Injili ya amani.
Chunguza Waefeso 6:14-15
7
Waefeso 6:10
Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.
Chunguza Waefeso 6:10
8
Waefeso 6:2-3
“Waheshimu baba yako na mama yako,” hii ndio amri ya kwanza yenye ahadi, “upate baraka na uishi siku nyingi duniani.”
Chunguza Waefeso 6:2-3
9
Waefeso 6:1
Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, kwa kuwa hili ni jema.
Chunguza Waefeso 6:1
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video