Basi nikatabiri kama nilivyoamriwa. Nilipokuwa nikitabiri, kukawa na sauti, sauti ya kugongana, nayo mifupa ikasogeleana, mfupa kwa mfupa mwenziwe. Nikatazama: mishipa na nyama vikatokea juu ya mifupa na ngozi ikaifunika, lakini haikuwa na pumzi ndani yake.