Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, wala hakuna mwingine,
zaidi yangu hakuna Mungu.
Nitakutia nguvu,
ingawa wewe hujanitambua,
ili kutoka mawio ya jua
hadi machweo yake,
watu wapate kujua kwamba hakuna Mungu mwingine ila Mimi.
Mimi ndimi Mwenyezi Mungu wala hakuna mwingine.