1
Isaya 65:24
Neno: Bibilia Takatifu
Kabla hawajaita, nitajibu, nao wakiwa katika kunena, nitasikia.
Linganisha
Chunguza Isaya 65:24
2
Isaya 65:17
“Tazama, nitaumba mbingu mpya na dunia mpya. Mambo ya zamani hayatakumbukwa, wala hayatakuja akilini.
Chunguza Isaya 65:17
3
Isaya 65:23
Hawatajitaabisha kwa kazi bure, wala hawatazaa watoto ili wapatwe na majanga, kwa kuwa watakuwa taifa lililobarikiwa na BWANA, wao na wazao wao pamoja nao.
Chunguza Isaya 65:23
4
Isaya 65:22
Hawatajenga nyumba, nao watu wengine waishi ndani yake, au kupanda mazao na wengine wale. Kwa kuwa kama zilivyo siku za mti, ndivyo zitakavyokuwa siku za watu wangu, wateule wangu watafurahia kwa siku nyingi kazi za mikono yao.
Chunguza Isaya 65:22
5
Isaya 65:20
“Kamwe hatakuwepo tena ndani yake mtoto mchanga atakayeishi siku chache tu, au mzee ambaye hataishi akatimiza miaka yake. Yeye atakayekufa akiwa na umri wa miaka mia moja atahesabiwa kwamba ni kijana tu, yeye ambaye hatafika miaka mia moja, atahesabiwa kuwa amelaaniwa.
Chunguza Isaya 65:20
6
Isaya 65:25
Mbwa mwitu na mwana-kondoo watalisha pamoja, naye simba atakula nyasi kama maksai, lakini mavumbi yatakuwa chakula cha nyoka. Hawatadhuru wala kuharibu katika mlima wangu mtakatifu wote,” asema BWANA.
Chunguza Isaya 65:25
7
Isaya 65:19
Nami nitaifurahia Yerusalemu na kuwafurahia watu wangu; sauti ya maombolezo na ya kilio haitasikika humo tena.
Chunguza Isaya 65:19
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video