1
Marko 13:13
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Watu wote watawachukia kwa ajili ya Jina langu. Lakini yule atakayevumilia hadi mwisho ataokolewa.
Linganisha
Chunguza Marko 13:13
2
Marko 13:33
Jihadharini! Kesheni! Kwa maana hamjui wakati ule utakapowadia.
Chunguza Marko 13:33
3
Marko 13:11
Mtakapokamatwa na kushtakiwa, msisumbuke awali kuhusu mtakalosema. Semeni tu lolote mtakalopewa wakati huo, kwa kuwa si ninyi mtakaokuwa mkinena, bali ni Roho Mtakatifu wa Mungu.
Chunguza Marko 13:11
4
Marko 13:31
Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
Chunguza Marko 13:31
5
Marko 13:32
“Kwa habari ya siku ile na saa hakuna yeyote ajuaye, hata malaika walio mbinguni wala Mwana, ila Baba peke yake.
Chunguza Marko 13:32
6
Marko 13:7
Msikiapo habari za vita na uvumi wa vita, msiwe na hofu. Mambo haya hayana budi kutukia, lakini ule mwisho bado.
Chunguza Marko 13:7
7
Marko 13:35-37
“Basi kesheni, kwa sababu hamjui ni lini mwenye nyumba atakaporudi: iwapo ni jioni, au ni usiku wa manane, au alfajiri awikapo jogoo, au mapambazuko, akija ghafula asije akawakuta mmelala. Lile ninalowaambia ninyi, nawaambia watu wote: ‘Kesheni!’ ”
Chunguza Marko 13:35-37
8
Marko 13:8
Taifa litainuka dhidi ya taifa na ufalme dhidi ya ufalme. Kutakuwa na mitetemeko ya ardhi sehemu mbalimbali na njaa. Haya yatakuwa ndio mwanzo wa uchungu.
Chunguza Marko 13:8
9
Marko 13:10
Nayo Injili lazima ihubiriwe kwanza kwa mataifa yote.
Chunguza Marko 13:10
10
Marko 13:6
Wengi watakuja kwa Jina langu wakidai, ‘Mimi ndiye,’ nao watawadanganya wengi.
Chunguza Marko 13:6
11
Marko 13:9
“Lakini ninyi jihadharini. Kwa maana watawapeleka katika mabaraza yao na kupigwa mijeledi katika masinagogi. Mtashtakiwa mbele ya watawala na wafalme kwa ajili yangu, ili kuwa ushuhuda kwao.
Chunguza Marko 13:9
12
Marko 13:22
Kwa maana watatokea masihi wa uongo na manabii wa uongo, nao watafanya ishara na maajabu ili kuwapotosha, ikiwezekana, hata wale wateule.
Chunguza Marko 13:22
13
Marko 13:24-25
“Lakini katika siku hizo, baada ya hiyo dhiki, “ ‘jua litatiwa giza nao mwezi hautatoa nuru yake; nazo nyota zitaanguka kutoka angani, na nguvu za anga zitatikisika.’
Chunguza Marko 13:24-25
Nyumbani
Bibilia
Mipango
Video