Kwa hiyo, Mungu alimtukuza juu sana,
na kumpa Jina lililo kuu kuliko kila jina,
ili kwa Jina la Isa, kila goti lipigwe,
la vitu vya mbinguni, na vya duniani,
na vya chini ya nchi,
na kila ulimi ukiri kwamba
Isa Al-Masihi ni Bwana,
kwa utukufu wa Mungu Baba Mwenyezi.