1
Mithali 10:22
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Baraka ya Mwenyezi Mungu hutajirisha, wala haichanganyi na huzuni.
Linganisha
Chunguza Mithali 10:22
2
Mithali 10:19
Dhambi haiondolewi kwa maneno mengi, bali wenye busara huzuia ulimi wao.
Chunguza Mithali 10:19
3
Mithali 10:12
Chuki huchochea faraka, lakini upendo husitiri mabaya yote.
Chunguza Mithali 10:12
4
Mithali 10:4
Mikono mivivu hufanya mtu kuwa maskini lakini mikono yenye bidii huleta utajiri.
Chunguza Mithali 10:4
5
Mithali 10:17
Anayekubali kuadibishwa yuko katika njia ya uzima, lakini yeyote anayepuuza maonyo hupotosha wengine.
Chunguza Mithali 10:17
6
Mithali 10:9
Mtu mwadilifu hutembea salama, lakini mtu aendaye katika njia zilizopotoka atagunduliwa.
Chunguza Mithali 10:9
7
Mithali 10:27
Kumcha Mwenyezi Mungu huongeza urefu wa maisha, lakini miaka ya mwovu inafupishwa.
Chunguza Mithali 10:27
8
Mithali 10:3
Mwenyezi Mungu hawaachi waadilifu kukaa njaa, lakini hupinga tamaa ya mtu mwovu.
Chunguza Mithali 10:3
9
Mithali 10:25
Tufani inapopita, waovu hutoweka, lakini wenye haki husimama imara milele.
Chunguza Mithali 10:25
Nyumbani
Bibilia
Mipango
Video