1
Kumbukumbu la Torati 4:29
Swahili Revised Union Version
Lakini huko, kama mkimtafuta BWANA, Mungu wako, utampata, ukimtafuta kwa moyo wako wote, na roho yako yote.
Linganisha
Chunguza Kumbukumbu la Torati 4:29
2
Kumbukumbu la Torati 4:31
kwa kuwa BWANA, Mungu wako, ni Mungu wa rehema; hatakuacha wala kukuangamiza, wala hatalisahau agano la baba zako alilowaapia.
Chunguza Kumbukumbu la Torati 4:31
3
Kumbukumbu la Torati 4:24
kwa kuwa BWANA, Mungu wenu, ni moto uangamizao, Mungu mwenye wivu.
Chunguza Kumbukumbu la Torati 4:24
4
Kumbukumbu la Torati 4:9
Lakini, jihadhari nafsi yako, ukailinde roho yako kwa bidii, usije ukayasahau mambo yale uliyoyaona kwa macho yako, yakaondoka moyoni mwako siku zote za maisha yako; bali uwajulishe watoto wako na watoto wa watoto wako
Chunguza Kumbukumbu la Torati 4:9
5
Kumbukumbu la Torati 4:39
Kwa hiyo ujue, leo hivi, ukaweke moyoni mwako, ya kuwa BWANA ndiye Mungu katika mbingu juu, na katika nchi chini; hapana mwingine.
Chunguza Kumbukumbu la Torati 4:39
6
Kumbukumbu la Torati 4:7
Kwa maana liko taifa gani kubwa, lililo na Mungu aliye karibu nao, kama BWANA Mungu wetu alivyo kila tumwitapo?
Chunguza Kumbukumbu la Torati 4:7
7
Kumbukumbu la Torati 4:30
Na wakati uwapo katika mashaka, ukiisha kupatwa na mambo haya yote, siku za mwisho, utamrudia BWANA, Mungu wako, na kuisikiza sauti yake
Chunguza Kumbukumbu la Torati 4:30
8
Kumbukumbu la Torati 4:2
Msiliongeze neno ninalowaamuru wala msilipunguze, mpate kuzishika amri za BWANA, Mungu wenu, ninazowaamuru.
Chunguza Kumbukumbu la Torati 4:2
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video