Ghafula, sauti kama mvumo mkubwa wa upepo mkali ikatoka mbinguni, ikaijaza nyumba yote walimokuwa wameketi. Zikatokea ndimi kama za moto zilizogawanyika na kutua juu ya kila mmoja wao. Wote wakajazwa na Roho Mtakatifu wa Mungu, wakaanza kunena kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia.