Ndipo, Farao alipomwambia Yosefu kwamba: Baba yako na ndugu zako wamekuja kwako. Basi, nchi ya Misri iko wazi machoi pako; mkalishe baba yako pamoja na ndugu zako katika nchi iliyo nzuri zaidi! Na wakae katika nchi ya Goseni! Nao, uwajuao kuwa mafundi wa kazi hiyo, uwaweke kuwa wakuu wao wanaoyachunga makundi yangu.