1
Yohana 11:25-26
Neno: Maandiko Matakatifu
Isa akamwambia, “Mimi ndiye huo ufufuo na uzima. Yeye aniaminiye mimi, hata akifa atakuwa anaishi na yeyote aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je, unasadiki haya?”
Linganisha
Chunguza Yohana 11:25-26
2
Yohana 11:40
Isa akamwambia, “Sikukuambia kwamba kama ukiamini utauona utukufu wa Mungu?”
Chunguza Yohana 11:40
3
Yohana 11:35
Isa akalia machozi.
Chunguza Yohana 11:35
4
Yohana 11:4
Lakini Isa aliposikia hayo, akasema, “Ugonjwa huu hautaleta mauti bali umetokea ili kudhihirisha utukufu wa Mungu, ili Mwana wa Mungu apate kutukuzwa kutokana na ugonjwa huu.”
Chunguza Yohana 11:4
5
Yohana 11:43-44
Baada ya kusema haya, Isa akapaza sauti yake, akaita, “Lazaro, njoo huku!” Yule aliyekuwa amekufa akatoka nje, mikono yake na miguu yake ikiwa imeviringishiwa vitambaa vya kitani na leso usoni pake. Isa akawaambia, “Mfungueni, mwacheni aende zake.”
Chunguza Yohana 11:43-44
6
Yohana 11:38
Isa kwa mara nyingine akiwa amefadhaika sana, akafika penye kaburi. Hilo kaburi lilikuwa pango ambalo jiwe lilikuwa limewekwa kwenye ingilio lake.
Chunguza Yohana 11:38
7
Yohana 11:11
Baada ya kusema haya, Isa akawaambia, “Rafiki yetu Lazaro amelala, lakini naenda kumwamsha.”
Chunguza Yohana 11:11
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video