1
Yohana 14:27
Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Amani nawaachia; amani yangu nawapa. Amani hii ninayowapa si kama ile ulimwengu unatoa. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiogope.
Linganisha
Chunguza Yohana 14:27
2
Yohana 14:6
Isa akawaambia, “Mimi ndimi njia na kweli na uzima. Mtu hawezi kuja kwa Baba isipokuwa kupitia kwangu.
Chunguza Yohana 14:6
3
Yohana 14:1
Isa akawaambia, “Msifadhaike mioyoni mwenu. Mnamwamini Mungu, mniamini pia.
Chunguza Yohana 14:1
4
Yohana 14:26
Lakini huyo Msaidizi, yaani huyo Roho Mtakatifu wa Mungu, ambaye Baba atamtuma kwenu kwa Jina langu, atawafundisha mambo yote na kuwakumbusha yote niliyowaambia.
Chunguza Yohana 14:26
5
Yohana 14:21
Yeyote mwenye amri zangu na kuzishika ndiye anipendaye. Naye anipendaye atapendwa na Baba yangu, nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.”
Chunguza Yohana 14:21
6
Yohana 14:16-17
Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine akae nanyi milele. Huyo ndiye Roho wa kweli ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa sababu haumwoni wala haumjui. Ninyi mnamjua kwa kuwa yuko pamoja nanyi, naye anakaa ndani yenu.
Chunguza Yohana 14:16-17
7
Yohana 14:13-14
Nanyi mkiomba lolote kwa Jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba apate kutukuzwa katika Mwana. Mkiniomba lolote kwa Jina langu, nitalifanya.
Chunguza Yohana 14:13-14
8
Yohana 14:15
“Kama mnanipenda, mtazishika amri zangu.
Chunguza Yohana 14:15
9
Yohana 14:2
Nyumbani mwa Baba yangu kuna makao mengi. Kama sivyo, ningewaambia. Naenda kuwaandalia makao.
Chunguza Yohana 14:2
10
Yohana 14:3
Nami nikienda na kuwaandalia makao, nitarudi tena na kuwachukua mkae pamoja nami, ili mahali nilipo nanyi mpate kuwepo.
Chunguza Yohana 14:3
11
Yohana 14:5
Tomaso akamwambia, “Bwana, sisi hatujui unakoenda, tutaijuaje njia?”
Chunguza Yohana 14:5
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video