Mwanangu, ukiyakubali maneno yangu,
na kuyathamini maagizo yangu;
ukitega sikio lako kusikiliza hekima,
na kuuelekeza moyo wako upate ufahamu;
naam, ukiomba upewe busara,
ukisihi upewe ufahamu;
ukiitafuta hekima kama fedha,
na kuitaka kama hazina iliyofichika;
hapo utaelewa ni nini kumcha Mwenyezi-Mungu,
utafahamu maana ya kumjua Mungu.