Ezekieli 35
35
Unabii dhidi ya Edomu
1Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: 2“Mwanadamu, elekeza uso wako juu ya Mlima Seiri, utabiri dhidi yake 3na useme: ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Mimi ni kinyume nawe, ee Mlima Seiri, nami nitanyoosha mkono wangu dhidi yako na kukufanya ukiwa. 4Nitaifanya miji yako kuwa magofu nawe utakuwa ukiwa. Ndipo utakapojua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.
5“ ‘Kwa sababu ulificha moyoni uadui wa siku nyingi nawe ukawatoa Waisraeli wauawe kwa upanga wakati wa maafa yao, wakati adhabu yake ilipofikia kilele chake, 6kwa hiyo hakika kama niishivyo, asema Bwana Mungu Mwenyezi, nitakutia katika umwagaji damu nao utakufuatia. Kwa kuwa hukuchukia kumwaga damu, kumwaga damu kutakufuatia. 7Nitaufanya Mlima Seiri ukiwa na kuukatilia mbali na wote wanaokuja na wanaoenda. 8Nitaijaza milima yenu kwa watu wake waliouawa, wale waliouawa kwa upanga wataanguka juu ya vilima vyako na katika mabonde yako na katika makorongo yako yote. 9Nitakufanya ukiwa milele, watu hawataishi katika miji yako. Ndipo utakapojua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.
10“ ‘Kwa sababu umesema, “Mataifa haya mawili na nchi hizi zitakuwa zetu nasi tutazimiliki,” ingawa hata Mimi Mwenyezi Mungu nilikuwa huko, 11kwa hiyo hakika kama niishivyo, asema Bwana Mungu Mwenyezi, nitakutenda kwa kadiri ya hasira na wivu uliouonesha katika chuki yako juu yao nami nitafanya nijulikane miongoni mwao wakati nitakapokuhukumu. 12Ndipo utakapojua kuwa Mimi Mwenyezi Mungu nimesikia mambo yote ya dharau uliyosema dhidi ya milima ya Israeli. Ulisema, “Wamefanyika ukiwa na kutiwa mikononi mwetu tuwararue.” 13Ulijigamba dhidi yangu na kusema maneno dhidi yangu bila kujizuia, nami nikayasikia. 14Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Dunia yote inaposhangilia, nitakufanya ukiwa. 15Kwa sababu ulishangilia wakati urithi wa nyumba ya Israeli ulipofanyika ukiwa, hivyo ndivyo nitakavyokutendea. Utakuwa ukiwa, ee Mlima Seiri, wewe na Edomu yote. Kisha ndipo watajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.’ ”
Iliyochaguliwa sasa
Ezekieli 35: NENO
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
![None](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapistaging.com%2F58%2Fhttps%3A%2F%2Fweb-assets.youversion.com%2Fapp-icons%2Fsw.png&w=128&q=75)
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Maandiko Matakatifu™ NMM™
Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa.
Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Scriptures™
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.