Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwanzo 36

36
Wazao wa Esau
(1 Nyakati 1:34-42)
1Hivi ndivyo vizazi vya Esau (yaani Edomu).
2Esau akaoa wake kutoka miongoni mwa wanawake wa Kanaani: Ada binti Eloni Mhiti, Oholibama binti Ana, mjukuu wa kike wa Sibeoni Mhivi; 3pia akaoa Basemathi binti Ishmaeli, dada yake Nebayothi.
4Ada akamzalia Esau Elifazi; Basemathi akamzaa Reueli; 5Oholibama akawazaa Yeushi, Yalamu na Kora. Hawa ndio wana wa Esau waliozaliwa kwake huko Kanaani.
6Esau akawachukua wake zake, watoto wake wa kiume na wa kike, na watu wote wa nyumbani mwake, mifugo yake pamoja na wanyama wake wengine wote, na mali yake yote ambayo alikuwa ameipata akiwa Kanaani, akahamia katika nchi iliyo mbali na Yakobo ndugu yake. 7Mali yao ilikuwa nyingi sana kiasi kwamba haikuwa rahisi wao kuishi pamoja; nchi waliyokuwa wakiishi isingewatosha wote kwa ajili ya mifugo yao. 8Kwa hiyo Esau (ambaye ni Edomu) aliishi katika nchi ya vilima ya Seiri.
9Hivi ndivyo vizazi vya Esau, baba wa Waedomu, katika nchi ya vilima ya Seiri.
10Haya ndiyo majina ya wana wa Esau:
Elifazi, mwana wa Esau ambaye mkewe Ada alimzalia; na Reueli, mwana wa Esau ambaye mkewe Basemathi alimzalia.
11Wana wa Elifazi ni:
Temani, Omari, Sefo, Gatamu na Kenazi. 12Elifazi mwana wa Esau alikuwa pia na suria aliyeitwa Timna, aliyemzalia Amaleki. Hao walikuwa wajukuu wa Ada mke wa Esau.
13Wana wa Reueli ni:
Nahathi, Zera, Shama na Miza. Hao walikuwa wajukuu wa Basemathi mkewe Esau.
14Wana wa Oholibama binti Ana, mkewe Esau, aliyekuwa mjukuu wa Sibeoni, aliomzalia Esau ni:
Yeushi, Yalamu na Kora.
15Hawa walikuwa wakuu miongoni mwa wazao wa Esau:
Wakuu wa wana wa Elifazi, mzaliwa wa kwanza wa Esau ni:
Temani, Omari, Sefo, Kenazi, 16Kora, Gatamu na Amaleki. Hao walikuwa wakuu waliotoka kwa Elifazi huko Edomu; walikuwa wajukuu wa kiume wa Ada.
17Wakuu wa wana wa Reueli, mwana wa Esau ni:
Nahathi, Zera, Shama na Miza. Hawa ndio wakuu waliotoka kwa Reueli huko Edomu; walikuwa wajukuu wa kiume wa Basemathi mkewe Esau.
18Wakuu wa wana wa Esau ambao mkewe Oholibama alimzalia ni:
Yeushi, Yalamu na Kora. Hawa ndio wakuu waliotoka kwa mke wa Esau, Oholibama binti Ana.
19Hao walikuwa wana wa Esau (ndiye Edomu), na hao walikuwa wakuu wao.
20Hawa walikuwa wana wa Seiri Mhori, walioishi katika nchi ile:
Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana, 21Dishoni, Eseri na Dishani. Hawa ndio wana wa Seiri huko Edomu waliokuwa wakuu kwa Wahori.
22Wana wa Lotani walikuwa:
Hori na Homamu. Timna alikuwa dada yake Lotani.
23Wana wa Shobali walikuwa:
Alvani, Manahathi, Ebali, Shefo na Onamu.
24Wana wa Sibeoni walikuwa:
Aya na Ana. (Huyu Ana ndiye aligundua chemchemi ya maji moto jangwani alipokuwa akichunga punda wa Sibeoni, baba yake.)
25Watoto wa Ana walikuwa:
Dishoni na Oholibama binti Ana.
26Wana wa Dishoni walikuwa:
Hemdani, Eshbani, Ithrani na Kerani.
27Wana wa Eseri walikuwa:
Bilhani, Zaavani na Akani.
28Wana wa Dishani walikuwa:
Usi na Arani.
29Hawa walikuwa wakuu wa Wahori:
Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana, 30Dishoni, Eseri na Dishani.
Hao walikuwa wakuu wa Wahori, kufuatana na makundi yao, katika nchi ya Seiri.
Watawala wa Edomu
(1 Nyakati 1:43-54)
31Wafuatao ni wafalme waliotawala Edomu kabla ya mfalme yeyote wa Israeli kutawala:
32Bela mwana wa Beori alikuwa mfalme wa Edomu. Mji wake uliitwa Dinhaba.
33Bela alipofariki, Yobabu mwana wa Zera kutoka Bosra akawa mfalme baada yake.
34Yobabu alipofariki, Hushamu kutoka nchi ya Watemani akawa mfalme baada yake.
35Hushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi, aliyeshinda Midiani katika nchi ya Moabu, akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Avithi.
36Hadadi alipofariki, Samla kutoka Masreka akawa mfalme baada yake.
37Samla alipofariki, Shauli kutoka Rehobothi ng’ambo ya Mto Frati akawa mfalme baada yake.
38Shauli alipofariki, Baal-Hanani mwana wa Akbori akawa mfalme baada yake.
39Baal-Hanani mwana wa Akbori alipofariki, Hadadi akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Pau, na mkewe aliitwa Mehetabeli binti Matredi, binti Me-Zahabu.
40Hawa ndio wakuu waliotokana na Esau, kwa majina, kufuatana na koo zao na nchi zao:
Timna, Alva, Yethethi,
41Oholibama, Ela, Pinoni,
42Kenazi, Temani, Mibsari,
43Magdieli na Iramu.
Hao walikuwa wakuu wa Edomu, kufuatana na makazi yao katika nchi waliyoimiliki.
Hivi ndivyo vizazi vya Esau, baba wa Waedomu.

Iliyochaguliwa sasa

Mwanzo 36: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia