Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maombolezo 3:21-33

Maombolezo 3:21-33 NEN

Hata hivyo najikumbusha neno hili na kwa hiyo ninalo tumaini. Kwa sababu ya upendo mkuu wa BWANA, hatuangamii, kwa kuwa huruma zake hazikomi kamwe. Ni mpya kila asubuhi, uaminifu wako ni mkuu. Nimeiambia nafsi yangu, “BWANA ni fungu langu, kwa hiyo nitamngojea.” BWANA ni mwema kwa wale ambao tumaini lao ni kwake, kwa yule ambaye humtafuta; ni vyema kungojea kwa utulivu kwa ajili ya wokovu wa BWANA. Ni vyema mtu kuchukua nira bado angali kijana. Na akae peke yake awe kimya, kwa maana BWANA ameiweka juu yake. Na azike uso wake mavumbini bado panawezekana kuwa na matumaini. Na atoe shavu lake kwa yule ampigaye, na ajazwe na aibu. Kwa kuwa watu hawakatiliwi mbali na Bwana milele. Ingawa huleta huzuni, ataonyesha huruma, kwa kuwa upendo wake usiokoma ni mkuu. Kwa maana hapendi kuwaletea mateso au huzuni watoto wa wanadamu.