Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Obadia 1:15-21

Obadia 1:15-21 NENO

“Siku ya Mwenyezi Mungu iko karibu kwa mataifa yote. Kama ulivyotenda, nawe utatendewa vivyo hivyo, matendo yako yatakurudia juu ya kichwa chako. Kama vile ulivyokunywa juu ya mlima wangu mtakatifu, vivyo hivyo mataifa yote watakunywa mfululizo; watakunywa na kunywa, nao watatoweka kana kwamba hawajawahi kuwepo. Lakini katika Mlima Sayuni kutakuwa na wale watakaookoka; nao utakuwa mtakatifu, nayo nyumba ya Yakobo itamiliki urithi wake. Nyumba ya Yakobo itakuwa moto, na nyumba ya Yusufu itakuwa mwali wa moto; nayo nyumba ya Esau itakuwa bua kavu, nao wataiwasha moto na kuiteketeza. Hakutakuwa na watakaosalimika kutoka nyumba ya Esau.” Mwenyezi Mungu amesema. Watu kutoka nchi ya Negebu wataimiliki milima ya Esau, na watu kutoka Shefela wataimiliki nchi ya Wafilisti. Watayamiliki mashamba ya Efraimu na Samaria, naye Benyamini atamiliki Gileadi. Kundi la Waisraeli walio uhamishoni Kanaani watarudi na kuimiliki nchi hadi Sarepta. Walio uhamishoni Sefaradi kutoka Yerusalemu wataimiliki miji ya Negebu. Waokoaji watakwea juu ya Mlima Sayuni kutawala milima ya Esau. Nao ufalme utakuwa wa Mwenyezi Mungu.

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha