Obadia Utangulizi
Utangulizi
Jina Obadia lina maana ya “Mtumishi wa Yehova.” Habari za nabii Obadia hazipatikani popote nje ya kitabu hiki. Unabii wa kitabu hiki unahusu hukumu ya Mwenyezi Mungu dhidi ya taifa la Edomu, na kukomeshwa na kuangamizwa kwa taifa hilo kwa sababu ya kiburi na udhalimu wake. Waedomu, waliokuwa uzao wa Esau, walijivunia usalama katika ngome zao kwenye Mlima Seiri, kusini mwa Bahari ya Chumvi. Askari wao walitumika katika jeshi la Nebukadneza baada ya Yerusalemu kutekwa na kuteketezwa mnamo 587 K.K. Waedomu waliwadharau watu wa Yuda, na hawakuwasaidia walipopatwa na mikasa ya kuvamiwa na kupigwa na majeshi ya kigeni. Mwanzoni mwa karne ya tisa, Waedomu wenyewe walishiriki zaidi ya mara nne kuiteka Yerusalemu.
Mwandishi
Obadia.
Kusudi
Kudhihirisha hasira kuu ya Mwenyezi Mungu na hukumu yake dhidi ya Waedomu.
Mahali
Yerusalemu.
Tarehe
Inadhaniwa kuwa mnamo 605–586 K.K.
Wahusika Wakuu
Waedomu.
Wazo Kuu
Hukumu ya Mwenyezi Mungu dhidi ya Waedomu.
Mambo Muhimu
Dharau, kiburi na udhalimu wa Waedomu na hukumu ya Mwenyezi Mungu kwao.
Yaliyomo
Maangamizi ya Edomu (1-14)
Kurejeshwa kwa Israeli (15-21).
Iliyochaguliwa sasa
Obadia Utangulizi: NENO
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Maandiko Matakatifu™ NMM™
Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa.
Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Scriptures™
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.