Zaburi 2:1-6
Zaburi 2:1-6 NENO
Kwa nini mataifa wanashauriana kufanya mabaya, na makabila ya watu kula njama bure? Wafalme wa dunia wanajipanga na watawala wanajikusanya dhidi ya Mwenyezi Mungu na dhidi ya Mpakwa Mafuta wake. Wanasema, “Tuvunje minyororo yao na kuvitupilia mbali vifungo vyao.” Yeye anayetawala mbinguni hucheka, Bwana huwadharau. Kisha huwakemea katika hasira yake na kuwaogopesha katika ghadhabu yake, akisema, “Nimemtawaza Mfalme wangu juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.”