Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 2:1-6

Zaburi 2:1-6 SRUV

Mbona mataifa yanafanya ghasia, Na watu kuwaza mambo ya bure? Wafalme wa dunia wanajipanga, Na wakuu wanafanya shauri pamoja, Juu ya BWANA, Na juu ya masihi wake, Na tuvipasue vifungo vyao, Na kuzitupa mbali nasi kamba zao. Yeye aketiye mbinguni anacheka, Bwana anawafanyia dhihaka. Ndipo atakaposema nao kwa hasira yake, Na kuwafadhaisha kwa ghadhabu yake, akisema: Nami nimemweka mfalme wangu Juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.

Soma Zaburi 2