Ruthu Utangulizi
Utangulizi
Kitabu hiki kimepewa jina la Ruthu, mhusika mkuu katika habari zilizoandikwa humu. Elimeleki na mkewe Naomi walilazimika kuhama kutoka Bethlehemu kwenda nchi ya Moabu. Muda mfupi baadaye, Elimeleki akafariki, nao wanawe Maloni na Kilioni wakaoa wanawake wa Kimoabu, Ruthu na Orpa. Maloni na Kilioni wakafariki bila watoto. Naomi alipoamua kurudi nyumbani mwake katika nchi ya Yuda, aliwashawishi wakwe wake kurudi kwao. Ruthu alisisitiza kwenda naye, lakini Orpa aliamua kurudi nyumbani.
Naomi na Ruthu walipofika Israeli, Ruthu alienda kutafuta riziki yao. Alijikuta katika mashamba ya mtu wa jamaa wa karibu wa Elimeleki, kwa jina Boazi, ambaye aliamuru Ruthu atunzwe na wafanyakazi wake. Baada ya muda, Boazi alimwoa Ruthu. Ukoo wa ufalme wa Israeli ulioanza na Mfalme Daudi ulitoka kwa ukoo huu. Baadaye Masihi, Isa Al-Masihi, anatajwa kuwa wa ukoo huu.
Mwandishi
Hajulikani, lakini mapokeo ya Kiyahudi yanasema Samweli ndiye mwandishi.
Kusudi
Kitabu cha Ruthu kinaonesha jinsi watu watatu wanaweza kuwa na mwenendo thabiti na wa uadilifu kwa Mwenyezi Mungu wakati jamii inayowazunguka imepotoka.
Mahali
Moabu na Bethlehemu.
Tarehe
Baada ya kipindi cha Waamuzi, kama 1050 K.K.
Wahusika Wakuu
Naomi, Ruthu na Boazi.
Wazo Kuu
Uhusiano kati ya Naomi na mkwewe Ruthu unatupatia kielelezo jinsi maisha ya kumcha Mwenyezi Mungu yanavyopaswa kuwa, na vile upendo wa kweli kwa jirani unavyoweza kuwa na matokeo ya baraka.
Mambo Muhimu
Kuambatana kwa Ruthu na Naomi kunaonesha uaminifu wa Ruthu, ijapokuwa Naomi alimsihi arudi kwa watu wake baada ya kufiwa na mumewe. Kutokana na uaminifu huo, Ruthu anatajwa katika uzao wa Isa kutokana na kuolewa na Boazi.
Yaliyomo
Naomi kuondoka Israeli, na kurudi kwake na Ruthu (1:1-22)
Ruthu anakaribishwa (2:1-23)
Ruthu na Boazi (3:1–4:22).
Iliyochaguliwa sasa
Ruthu Utangulizi: NENO
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Maandiko Matakatifu™ NMM™
Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa.
Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Scriptures™
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.