Zab 49:1-12
Zab 49:1-12 SUV
Sikieni haya, enyi mataifa yote; Sikilizeni, ninyi nyote mnaokaa duniani. Watu wakuu na watu wadogo wote pia, Tajiri na maskini wote pamoja. Kinywa changu kitanena hekima, Na fikira za moyo wangu zitakuwa za busara. Nitatega sikio langu nisikie mithali, Na kufumbua fumbo langu kwa kinubi Kwa nini niogope siku za uovu, Ubaya ukinizunguka miguuni pangu? Wa hao wanaozitumainia mali zao, Na kujisifia wingi wa utajiri wao; Hakuna mtu awezaye kumkomboa ndugu yake, Wala kumpa Mungu fidia kwa ajili yake, (Maana fidia ya nafsi zao ina gharama, Wala hana budi kuiacha hata milele;) ili aishi sikuzote asilione kaburi. Naam, ataliona, hata wenye hekima hufa; Mpumbavu na mjinga hupotea pamoja, Na kuwaachia wengine mali zao. Makaburi ni nyumba zao hata milele, Maskani zao vizazi hata vizazi. Hao waliotaja mashamba yao Kwa majina yao wenyewe. Lakini mwanadamu hadumu katika heshima, Bali amefanana na wanyama wapoteao.