Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 49:1-12

Zaburi 49:1-12 BHN

Sikieni jambo hili enyi watu wote! Tegeni sikio enyi wakazi wote wa dunia; sikilizeni nyote, wakubwa kwa wadogo, matajiri na maskini kwa pamoja. Maneno yangu yatakuwa mazitomazito; mimi nitasema maneno ya hekima. Nitatega sikio nisikilize methali, nitafafanua kitendawili kwa muziki wa zeze. Ya nini niogope siku mbaya, wakati nizungukwapo na uovu wa adui? Watu waovu hutegemea mali zao, hujisifia wingi wa utajiri wao. Lakini binadamu hawezi kamwe kujikomboa mwenyewe; hawezi kumlipa Mungu bei ya maisha yake, maana fidia ya maisha ni kubwa mno. Hawezi kutoa kitu chochote kinachotosha, kimwezeshe aendelee kuishi daima, asipate kuonja kaburi. Yeye afahamu kuwa hata wenye hekima hufa, wapumbavu hali kadhalika na watu wajinga. Wote hao huwaachia wengine mali zao. Makaburi ni makao yao hata milele; ni makao yao vizazi hata vizazi, ingawa hapo awali walimiliki ardhi. Binadamu hatadumu katika fahari yake; atakufa tu kama mnyama.

Soma Zaburi 49

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zaburi 49:1-12