Mithali 6:20-24
Mithali 6:20-24 SRUV
Mwanangu, shika maagizo ya baba yako, Wala usiiache sheria ya mama yako. Yafunge hayo katika moyo wako daima; Jivike hayo shingoni mwako. Uendapo yatakuongoza, ulalapo yatakulinda, Na uamkapo yatazungumza nawe. Maana maagizo hayo ni taa, na sheria hiyo ni nuru, Na maonyo ya kumwadilisha mtu ni njia ya uzima. Yakulinde na mwanamke mwovu, asikupate, Na kukuponya na ubembelezi wa mgeni.