Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mithali 8:1-21

Mithali 8:1-21 SRUV

Je! Hekima halii? Ufahamu hatoi sauti yake? Juu ya mahali palipoinuka karibu na njia, Penye njia panda, ndipo asimamapo. Karibu na malango, mahali pa kuingia mjini, Mahali pa kuyaingilia malango anapiga kelele. Enyi watu, nawaita ninyi; Na sauti yangu ni kwa wanadamu. Enyi wajinga, fahamuni werevu, Nanyi wapumbavu, mpate moyo wa kufahamu. Sikilizeni, maana nitasema yaliyo mazuri, Na kufumbua midomo yangu kutakuwa maadili. Maana kinywa changu kitasema kweli, Na uovu ni chukizo kwa midomo yangu. Maneno yote ya kinywa changu yana haki; Hapana hata neno lililopotoka au la ukaidi. Yote humwelea yule afahamuye, Yote huelekea mbele yao waliopata maarifa. Pokea mafundisho yangu, wala si fedha, Na maarifa kuliko dhahabu safi. Maana hekima ni bora kuliko marijani; Wala vyote vinavyotamanika havilingani nayo. Mimi, hekima, nimefanya werevu kuwa makao yangu; Natafuta maarifa na busara. Kumcha BWANA ni kuchukia uovu; Kiburi na majivuno, na njia mbovu, Na kinywa cha ukaidi pia nakichukia. Ushauri ni wangu, na maarifa yaliyo sahihi; Mimi ni ufahamu, mimi nina nguvu. Kwa msaada wangu wafalme humiliki, Na wakuu wanahukumu haki. Kwa msaada wangu wakuu hutawala, Na waungwana, naam, waamuzi wote wa dunia. Nawapenda wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona. Utajiri na heshima ziko kwangu, Naam, utajiri udumuo, na haki pia. Matunda yangu ni bora kuliko dhahabu, naam, dhahabu safi, Na faida yangu ni bora kuliko fedha iliyo safi. Natembea katika njia ya haki, Katikati ya mapito ya hukumu. Niwarithishe mali wale wanipendao, Tena nipate kuzijaza hazina zao.

Soma Mithali 8