Marko MT. 7
7
1KIISHA Mafarisayo na baadhi ya waandishi waliotoka Yerusalemi wakakusanyika mbele yake, 2wakaona baadhi ya wanafunzi wake wakila vyakula kwa mikono najis, yaani, yasiyonawiwa, wakawalaumu. 3Kwa maana Mafarisayo na Wayahudi wote wasiponawa mikono kwanza, hawali, wakishika hadithi za wazee wao: 4tena wakitoka sokoni, wasipotawadha, hawali; na yako mambo mengine waliyopokea kuyushika kama vile kuosha vikombe, na midumu, na vyombo vya shaba na meza. 5Bassi wale Mafarisayo na waandishi wakamwuliza, Mbona wanafunzi wako hawaendi kwa kuzifuata hadithi za wazee, bali hula chakula kwa mikono najis? 6Akawaambia, Isaya aliwakhubiri vema ninyi wanaliki, kama ilivyoandikwa,
Watu hawa hunibeshimu kwa midomo,
Bali mioyo yao iko mbali nami;
7Lakini waniabudu ibada ya burre,
Wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wana Adamu.
8Kwa maana mmeiacha amri ya Mungu, na kuzishika hadithi za wana Adamu, kuosha midumu na vikombe: na mengine mengi ya namna hii mwayafanya. 9Akawaambia, Mwaikataa vema amri ya Mungu mpate kushika hadithi zenu. 10Maana Musa alisema, Waheshimu baba yako na mama yako, na, Amtukanae baba yake au mama yake na afe. 11Bali ninyi hunena, Mtu akimwambia baba yake au mama yake, Ni Korban (yaani kimewekwa wakfu) kitu changu cho chote kikupasacho kufaidiwa nacho: 12wala hamrukhusu baada ya hayo kumtendea neno baba yake wala mama yake; 13mkilitangua neno la Mungu kwa hadithi yenu mliyohadithia; tena mwafanya mambo mengi yaliyo sawasawa na hayo. 14Akawaita makutano tena, akawaambia, Nisikieni nyote, fahamuni. 15Hapana kitu kilicho nje ya mtu ambacho kikimwingia chaweza kumtia najis, bali vimtokayo, ndivyo vimtiavyo najis yule mtu. 16Mtu akiwa na masikio ya kusikilia, na asikie. 17Hatta alipoingia nyumbani, amewaacha makutano, wanafunzi wake wakamwuliza khabari za ule mfano. 18Akawaambia, Hivi na ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kuwa killa kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia najis; 19kwa sababu hakimwingii moyoni, illa tumboni tu; kiisha chatoka kwenda chooni? Kwa kusema hivi alivitakasa vyakula vyote. 20Akanena, Kimtokacho mtu ndicho kimtiacho najis. 21Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, zina, asharati, 22wizi, uuaji, tamaa mbaya, hila, jeuri, kijicho, matukano, kiburi, upumbafu. 23Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu najis.
24Akaondoka huko, akaenda zake hatta mipaka ya Turo na Sidon. Akaingia katika nyumba, akataka isijulikane na mtu; lakini hakuweza kustirika. 25Kwa sababu mwanamke, ambae binti yake yuna pepo mchafu, alisikia khabari zake, akaja akamwangukia miguu. 26(Na vule mwanamke ni Myunani, kabila yake Msurofenissa). Akamwomba amfukuze pepo katika binti yake.
27Akamwambia, Waache watoto washibe kwanza: maana si vema kukitwaa chakula cha watoto, na kuwatupia mbwa. 28Nae akajibu, akamwambia, Naam, Bwana, lakini hatta mbwa chini ya meza hula makombo ya watoto. 29Akamwambia, Kwa sababu ya neno hilo, nenda zako; pepo amemtoka binti yako. 30Akaenda zake nyumbani kwake, akamkuta yule kijana amelazwa kitandani, na yule pepo amekwisha kumtoka.
31Akatoka tena katika mipaka ya Turo akapita katikati ya Sidon, akaenda hatta bahari ya Galilaya, kati ya mipaka ya Dekapoli. 32Wakamletea kiziwi, nae ana kigugumizi, wakamsihi aweke mikono yake juu yake. 33Akamtenga na makutano kwa faragha, akatia vidole vyake masikioni mwake, akatema mate, akamgusa nlimi, 34akatazama juu mbinguni, akaugua, akamwambia, Effatha, maana yake, Funguka! 35Marra masikio yake yakafunguka, kifungo cha ulimi wake kikalegea, akasema vizuri. 36Akawaagiza wasimwambie mtu; lakini kwa kadiri alivyozidi kuwaagiza, ndivyo walivyozidi kutangaza khabari, wakashangaa mno kupita kiasi, wakinena, 37Ametenda yote vizuri; viziwi awafanya wasikie, na bubu waseme.
Iliyochaguliwa sasa
Marko MT. 7: SWZZB1921
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.