Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Marko MT. 8

8
1TENA siku zile, kwa kuwa mengi mno makutano, nao hawana kitu cha kula, Yesu akawaita wanafunzi wake, akawaambia, 2Nawahurumia makutano kwa sababu yapata siku tatu wamekaa nami, wala hawana kitu cha kula: 3hatta nikiwaaga waende zao nyumbani kwao wanafunga, watazimia njiani: na baadhi yao wametoka mbali. 4Wanafunzi wake wakamjibu, Atawezaje mtu kuwashibisha hawa mikate hapa nyikani? 5Akawauliza, Mikate mingapi mnayo? Wakasenia, Saba. 6Akawaagiza makutano waketi chini: akaitwaa ile mikate saba, akashukuru, akaimega, akawapa wanafunzi wake wawaandalie: wakawaandalia makutano, 7Walikuwa na visamaki vichache; akavibariki, akasema, na hivi waviandae. 8Wakala, wakashiba, wakakusanya mabaki ya vipande vya mikate makanda saba. 9Na watu waliokula wapata elfu nne. Akawaaga. 10Marra akapanda chomboni pamoja na wanafunzi wake, akaenda pande za Dalmanutha.
11Wakatokea Mafarisayo wakaanza kuhujiana nae; wakitafuta kwake ishara itokayo mbinguni; wakimjaribu. 12Akaugua rohoni mwake, akanena, Mbona kizazi hiki chatafuta ishara? Amin, nawaambieni, Hakitapewa ishara kizazi hiki. 13Akawaacha, akapanda tena chomboni, akaenda zake hatta ngʼambu. 14Wakasahan kuchukua mikate, wala chomboni hawana illa mkate mmoja tu. 15Akawaagiza, akisema, Angalieni, jihadharini na chachu ya Mafarisayo na chachu ya Herode. 16Wakabishana wao kwa wao, kwa kuwa hawana mikate. 17Yesu akafahamu, akawaambia, Mbona mnabishana kwa sababu hamna mikate? Hamfahamu bado, wala hamjaelewa? Mioyo yenu i migumu hatta sasa? 18Mna macho, hamwoni; mna masikio, hamsikii? wala hamkumbuki? 19Nilipoimega ile mikate mitano na kuwapa wale elfu tano, mlichukua vikapu vingapi vimejaa vipande? Wakamwambia, Thenashara. 20Na ile saba kuwapa wale elfu nne, mlichukua makanda mangapi yamejaa vipande? Wakamwambia, Saba. 21Akawaambia, Imekuwaje hamjafahamu?
22Wakalika Bethsaida, wakamletea kipofu, wakamsihi amguse. 23Akamshika mkono vule kipofu, akamchukua nje ya kijiji, akamtemea mate ya macho, akaweka mikono yake juu yake, akamwuliza, Waona kitu? 24Akatazama juu, akanena, Naona watu kama miti, inakwenda. 25Ndipo akaweka mkono wake juu yake marra ya pili machoni mwake, akamwagiza atazame juu; akapata kuwa mzima, akaona wote waziwazi, wajapokuwa mbali. 26Akampeleka nyumbani kwake, akinena, Usiingie mjini, wala usiseme na mtu mjini.
27Akatoka Yesu na wanafunzi wake wakaenda vijiji vya Kaisaria ya Filipo: hatta njiani akawauliza wanafunzi wake, akiwaambia, Watu huninena mimi ni nani? 28Wakamjibu, Yohana Mbatizaji; wengine Eliya; wengine mmojawapo wa manabii. 29Yeye akawauliza, Na ninyi mnasema ya kuwa mimi ni nani? Petro akamjibu akamwambia, Wewe ndiwe Kristo. 30Akawaagiza wasimwambie mtu khabari zake. 31Akaanza kuwafundisha kwamba imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso mengi, na kukataliwa na wazee, na makuhani, wakuu na waandishi, na kuuawa, na baada ya siku tatu kufufuka. 32Petro akamchukua akaanza kumkemea. 33Akageuka akawatazama wanafunzi wake, akamkemea Petro, akinena, Enenda zako nyuma yangu, Shetani; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, hali ya wana Adamu. 34Akawaita makutano na wanafunzi wake, akawaambia, Atakae kuniandama na ajikane nafsi yake, ajitwike msalaba wake, anifuate. 35Kwa maana atakae kuisalimisha roho yake, ataiangamiza, na mtu atakaeitoa roho yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya injili, huyu ataisalimisha. 36Maana itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote akapata khasara ya roho yake? 37Ama mtu atoe nini badala ya roho yake? 38Maana killa mtu atakaenionea haya mimi, na maneno yangu, katika kizazi hiki cha zina na dhambi, Mwana wa Adamu atamwonea haya yeye atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu.

Iliyochaguliwa sasa

Marko MT. 8: SWZZB1921

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia