Marko MT. 9
9
1AKAWAAMBIA, Amin, nawaambieni, Pana watu katika hawa wasimamao hapa ambao hawataonja mauti hatta watakapouona ufalme wa Mungu umekuja kwa nguvu.
2Hatta baada ya siku sita Yesu akawachukua Petro, na Yakobo, na Yohana, akawapeleka juu ya mlima mrefu kwa faragha peke yao: 3akageuka sura yake mbele yao: mavazi yake yakawa yakimetameta, meupe kwa mfano wa thuluji, jinsi asivyoweza fundi duniani kuyafanya meupe. 4Wakatokewa na Eliya pamoja na Musa, nao walikuwa wakisemezana na Yesu. 5Petro akajibu, akamwambia Yesu, Rabbi, ni vizuri sisi kuwapo hapa: na tufanye vibanda vitatu, kimoja chako wewe, kimoja cha Musa, na kimoja eha Eliya. 6Maana yake hakujua la kunena, kwa kuwa waliingiwa na khofu nyingi. 7Likawako wingu, likawatia uvuli: sauti ikatoka katika lile wingu, Huyu ui Mwana wangu, mpendwa wangu, msikieni yeye. 8Na marra hiyo walipotazama huku na huku, hawakumwona mtu, illa Yesu peke yake pamoja nao.
9Walipokuwa wakishuka mlimani akawaagiza wasimweleze mtu waliyoyaona, illa Mwana wa Adamu atakapokuwa amefufuka katika wafu. 10Wakalishika neno lile, wakiulizana wao kwa wao, Huku kufufuka katika wafu maana yake nini? 11Wakamhoji, wakinena, Waandishi wanena ya kuwa imempasa Eliya kuja kwanza. 12Akajihu akawaambia, Ni kweli Eliya yuaja kwanza, na kutengeneza yote; lakini, pamoja na haya ameandikwaje Mwana wa Adamu ya kwamba atateswa mengi na kudharanliwa? 13Lakini nawaambieni, Eliya amekwisha kuja, nao wakamtenda yote waliyoyataka kama alivyoandikiwa. 14Hatta alipowafikia wanafunzi wake, akaona makutano mengi wakiwazunguka na waandishi wakijadiliana nao; 15marra makutano yote wakimwona wakashangaa wakamwendea mbio, wakamsalimu. 16Akawauliza wale waandishi, Nini mnajadiliana nao? 17Mtu mmoja katika makutano akamjibu, Nalimieta mwana wangu kwako, ana pepo bubu: 18na killa ampagaapo, humrarua: nikasema na wanafunzi wako wapate kumfukuza, wasiweze. 19Akamjibu, akanena, Ee kizazi kisichoamini, niwe kwenu hatta lini? nichukuliane nanyi hatta lini? Mleteni kwangu. 20Wakanileta kwake: hatta alipomwona marra yule pepo akamrarua: akaanguka chini, akagaagaa, akitoka povu. 21Akamwuliza baba yake, Tangu wakati gani amepatwa na haya? Akasema, Tangu utoto. 22Na marra nyingi amemtupa katika moto, na katika maji, amwangamize; lakini ukiweza neno, utuhurumie, utusaidie. 23Yesu akamwambia, Ukiweza kuamini: yote yawezekana kwake aaminiye. 24Marra baba yake yule kijana akapaaza sauti, machozi yakimtoka, akanena, Naamini, Bwana, nisaidie kutokuamini kwangu. 25Nae Yesu akiona ya kuwa makutano yanakusanyika mbio, akamkemea yule pepo mchafu, akamwambia, Ewe pepo bubu ua kiziwi, mimi nakuamuru, mtoke, wala usimwingie tena. 26Akalia, akamrarua sana, akamtoka: akawa kama amekufa: hatta wengi wakasema, Amekufa. 27Lakini Yesu akamshika mkouo akamwinua; nae akasimama. 28Hatta alipoingia nyumbani, wanafunzi wake wakamwuliza kwa faragha, Mbona sisi hatukuweza kumfukuza? 29Akawaambia, Namna hii haiwezi kutoka kwa neno lo lote, isipokuwa kwa kusali na kufunga. 30Wakatoka huko, wakapita kati kati ya Galilaya: nae hakutaka mtu ajue. 31Kwa sababu alikuwa akiwafundisha wanafunzi wake, akiwaambia ya kwamba Mwana wa Adamu anakwenda kutiwa katika mikono ya watu, nao watamwua; hatta akiisha kuuawa, baada ya siku tatu atafufuka. 32Nao hawakulifahamu neno lile, wakaogopa kumwuliza.
33Wakafika Kapernaum: hatta alipokuwa nyumbani, akawauliza, Mlishindania nini njiani? 34Wakanyamaza. Kwa maana walikuwa wakibishana wao kwa wao, ni nani aliye mkubwa. 35Akaketi chini akawaita wathenashara akawaambia, Mtu atakae kuwa wa kwanza atakuwa wa mwisho kuliko wote, na mkhudumu wa wote. 36Akatwaa kitoto, akamweka kati kati yao, akamkumbatia, akawaambia, 37Mtu akimpokea kitoto kimoja wa namna hii kwa jina langu, anipokea mimi: na mtu akinipokea mimi, hanipokei mimi, bali yeye aliyenituma.
38Yohana akamjibu, akamwambia, Mwalimu, tulimwona mtu akifukuza pepo kwa jina lako, nae hatufuati sisi: tukamkataza, kwa sababu hatufuati sisi. 39Yesu akasema, Msimkataze, kwa kuwa hakuna mtu atakaefanya mwujiza kwa jina langu akaweza wakati huo huo kuninena mabaya; 40kwa sababu asiye kiuyume chetu, ni upande wetu. 41Kwa kuwa ye yote atakaewanywesha ninyi kikombe cha maji kwa jina langu, kwa kuwa ninyi watu wa Kristo, amin nawaambieni hatakosa thawabu yake. 42Na ye yote atakaemkosesha mmoja katika wadogo hawa waniaminio, afadhali afungiwe jiwe la kusagia shingoni mwake, na kutupwa baharini. 43Na mkono wako ukikukosesha, ukate; ni kheri kuiingia katika uzima u kilema, kuliko kuwa na mikono miwili, na kwenda zako jehannum, kwenye moto usiozimika; 44ambao funza wao hafi, wala moto hauzimiki. 45Na mguu wako ukikukosesha, ukate: ni kheri kuingia katika uzima, umepungukiwa mguu, kuliko kuwa na miguu miwili, na kutupwa katika jebannum, katika moto usiozimika; 46ambao funza wao hafi, wala moto hauzimiki. 47Na jicho lako likikukosesha, litupe: ni kheri kuingia katika ufalme wa Mungu, una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehannum ya moto: 48ambapo funza wao hafi, wala moto hauzimiki. 49Kwa sababu killa mtu atatiwa chumvi kwa moto, na killa dhabihu itatiwa chumvi kwa chumvi. 50Chumvi ni njema; lakini chumvi ikitokwa na ladhdha yake, mtaitia nini ikolee? Mwe na chumvi ndani yenu, mkakae kwa amani ninyi kwa ninyi.
Iliyochaguliwa sasa
Marko MT. 9: SWZZB1921
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.