2 Mose 6
6
Bwana anamtokea Mose tena.
1Bwana akamwambia Mose: Sasa utayaona, nitakayomfanyizia Farao, kwani kwa mkono wenye nguvu atawapa ruhusa kwenda zao, tena kwa huo mkono wenye nguvu atawakimbiza, waitoke nchi yake.#2 Mose 11:1; 12:33.
2Kisha Bwana akasema na Mose, akamwambia: Mimi ni Bwana. 3Nilimtokea Aburahamu na Isaka na Yakobo, wanijue kuwa Mungu Mwenyezi, lakini Jina langu la Bwana sikulijulisha kwao.#1 Mose 17:1; 2 Mose 3:14-15; 1 Mose 12:7. 4Nalo Agano langu, nililolifanya nao, nitalisimamisha, lile la kuwapa nchi ya Kanaani, ndiyo nchi, waliyoikaa ugeni ni kwani walikuwa wageni huko. 5Nami niliposikia, wana wa Isiraeli wanavyopiga kite kwa hivyo, Wamisri wanavyowafanyizisha kazi za utumwa, nimelikumbuka hilo Agano langu. 6Kwa sababu hii waambie wana wa Isiraeli: Mimi ni Bwana, mimi nitawatoa Misri na kuwatua mizigo yenu, mimi nitawatoa utumwani mwenu na kuwakomboa ninyi kwa kuukunjua mkono na kwa mapatilizo makubwa. 7Nami nitawachukua ninyi, mwe ukoo wangu, nami nitakuwa Mungu wenu, nanyi mtatambua, ya kuwa mimi Bwana ni Mungu wenu aliyewatoa Misri na kuwatua mizigo yenu. 8Nami nitawapeleka katika hiyo nchi, niliyoiapia na kuuinua mkono wangu kwamba: Nitampa Aburahamu na Isaka na Yakobo; hiyo ndiyo, mimi Bwana nitakayowapa ninyi, iwe yenu.#1 Mose 22:16; 5 Mose 32:40. 9Mose alipowaambia wana wa Isiraeli maneno haya, hawakumsikia Mose, kwa kuwa roho zao zilikuwa zimesongeka, kazi zikizidi kuwa ngumu.
10Kisha Bwana akamwambia Mose kwamba: 11Nenda, useme na Farao, mfalme wa Misri, awape wana wa Isiraeli ruhusa kutoka katika nchi yake! 12Lakini Mose akamwambia Bwana waziwazi kwamba: Tazama! Wana wa Isiraeli wasiponisikia, Farao atanisikiaje mimi niliye mwenye midomo isiyofunguliwa kusema vema?#2 Mose 6:30; 4:10. 13Kisha Bwana akasema nao Mose na Haroni akiwaagiza kwenda kwa wana wa Isiraeli na kwa Farao, mfalme wa Misri, wapate kuwatoa wana wa Isiraeli katika nchi ya Misri.
Ndugu zao Haroni na Mose.
14Hawa ndio vichwa vya milango ya baba zao: Wana wa Rubeni aliyekuwa mzaliwa wa kwanza wa Isiraeli ndio hawa: Henoki na Palu, Hesironi na Karmi. Hizi ndizo ndugu zao wa Rubeni.#1 Mose 46:9-11. 15Nao wana wa Simeoni ndio hawa: Yemueli na Yamini na Ohadi na Yakini na Sohari na Sauli, mwana wa mke wa Kikanaani. Hizi ndizo ndugu zao wa Simeoni. 16Nayo haya ndiyo majina ya wana wa Lawi, kama walivyofuatana kuzaliwa: Gersoni na Kehati na Merari, nayo miaka ya kuwapo kwake Lawi ilikuwa miaka 137.#1 Mambo 6:1-4,16-19. 17Wana wa Gersoni ni Libuni na simei kwa udugu wao. 18Nao wana wa Kehati ni Amuramu na Isihari na Heburoni na Uzieli; nayo miaka ya kuwapo kwake Kehati ilikuwa miaka 133. 19Nao wana wa Merari ni Mahali na Musi; hizi ndio ndugu zao Walawi kwa hiyo, walivyofuatana kuzaliwa. 20Naye Amuramu akaamchukua Yokebedi aliyekuwa shangazi yake kuwa mkewe, naye akamzalia Haroni na Mose; nayo miaka ya kuwapo kwake Amuramu ilikuwa miaka 137. 21Nao wana wa Isihari ni Kora na Nefegi na Zikiri.#4 Mose 16:1. 22Nao wana wa Uzieli ni Misaeli na Elsafani na Sitiri. 23Naye Haroni akamchukua Eliseba, binti Aminadabu, umbu lake Nasoni, kuwa mkewe, naye akamzalia Nadabu na Abihu na Elazari na Itamari.#3 Mose 10:4; 2 Mose 28:1. 24Nao wana wa Kora ni Asiri na Elkana na Abiasafu. Hizi ndizo ndugu zao Wakora. 25Naye Elazari, mwana wa Haroni, akachukua mmoja wao wana wa Putieli kuwa mkewe, naye akamzalia Pinehasi. Hawa ndio vichwa vya milango ya baba zao Walawi kwa udugu wao.#4 Mose 25:7. 26Yule Haroni naye yule Mose ndio, Bwana aliowaambia: Watoeni wana wa Isiraeli katika nchi hii ya Misri kikosi kwa kikosi! 27Wao ndio waliosema na Farao, mfalme wa Misri, wapate kuwatoa wana wa Isiraeli huko Misri, yeye Mose naye Haroni.
28Ikawa siku hiyo, Bwana aliposema na Mose huko Misri, 29ndipo, Bwana alipomwambia Mose kwamba: Mimi ni Bwana; mwambie Farao, mfalme wa Misri, yote, mimi nitakayokuambia; 30tena ndipo hapo, Mose alipomwambia Bwana waziwazi: Tazama, mimi ni mwenye midomo isiyofunguliwa kusema vema; kwa hiyo Farao atanisikiaje?#2 Mose 6:12.
Iliyochaguliwa sasa
2 Mose 6: SRB37
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
![None](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapistaging.com%2F58%2Fhttps%3A%2F%2Fweb-assets.youversion.com%2Fapp-icons%2Fsw.png&w=128&q=75)
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.