Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Mose 25

25
Aburahamu anaoa mara ya pili.
1Aburahamu akaoa tena, jina lake mkewe ni Ketura.#1 Mambo 1:32-33. 2Huyu akamzalia Zimurani na Yokisani na Medani na Midiani na Isibaki na Sua. 3Naye Yokisani akamzaa Saba na Dedani; nao wana wa Dedani walikuwa Waasuri na Waletusi na Walumu. 4Nao wana wa Midiani walikuwa Efa na Eferi na Henoki na Abida na Eldaa; hawa wote walikuwa wana wa Ketura. 5Kisha Aburahamu akampa Isaka yote pia, aliyokuwa aliyo. 6Lakini wana wa masuria, Aburhamu aliokuwa nao, Aburahamu akawapa matunzo, kisha akawatuma angaliko mzima kuondoka kwa mwanawe Isaka, waende upande wa maawioni kwa jua kukaa katika nchi ya huko maawioni kwa jua.
Kufa na kuzikwa kwake Aburahamu.
7Siku zote za miaka ya kuwapo kwake Aburahamu, aliyokuwapo, ni miaka 175. 8Kisha Aburahamu akazimia, akafa kwa kuwa mkongwe sana, naye alikuwa mzee aliyeshiba siku zake; ndipo, alipochukuliwa kwenda kwao walio wa ukoo wake.#1 Mose 15:15; Iy. 5:26. 9Wanawe Isaka na Isimaeli wakamzika mle pangoni mwa Makipela katika shamba la Yule Mhiti Efuroni, mwana wa Sohari, linaloelekea Mamure. 10Ndilo lile shamba, Aburahamu alilolinunua kwa wana wa Hiti; ndiko, Aburahamu alikozikwa na mkewe Sara.#1 Mose 23:16-17. 11Aburahamu alipokwisha kufa, Mungu akambariki mwanawe Isaka. Naye Isaka akakaa kwenye kisima cha Mwenye Uzima Anionaye.#1 Mose 24:62.
Vizazi vya Isimaeli.
12Hivi ndiyo vizazi vya Isimaeli, mwana wa Aburahamu, ambaye Hagari wa Misri aliyekuwa kijakazi wake Sara alimzalia Aburahamu.#1 Mose 21:13. 13Nayo haya ndiyo majina ya wana wa Isimaeli waliyoitwa hivyo, walivyofuatana kuzaliwa: Mwana wa kwanza wa Isimaeli ni Nebayoti, tena Kedari na Adibeli na Mibusamu,#1 Mambo 1:29-31. 14na Misima na Duma na Masa; 15Hadadi na Tema, Yeturi, Nafisi na Kedima.#1 Mose 17:20. 16Hawa ndio wana wa Isimaeli, nayo haya ndiyo majina yao, waliyoitwa katika vijiji vyao na katika makambi ya mahema yao; nao walikuwa wakuu 12 wa makabila yao. 17Nayo hii ndiyo miaka ya kuwapo kwake Isimaeli, miaka 137; kisha akazimia, akafa, akachukuliwa kwenda kwao walio wa ukoo wake. 18Nao wale walikaa toka Hawila mpaka Suri unaoelekea Misri hata kufika Asuri; hivyo alikuwa ametua mbele yao ndugu zake wote.#1 Mose 16:12.
Kuzaliwa kwao Esau na Yakobo.
19Hivi ndivyo vizazi vya Isaka, mwana wa Aburahamu: Aburahamu alimzaa Isaka. 20Isaka alikuwa mwenye miaka 40 alipomchukua Rebeka kuwa mkewe, naye alikuwa binti Betueli, Mshami na Mesopotamia, dada yake Mshami Labani. 21Isaka akamwombea mkewe kwake Bwana, kwani alikuwa mgumba; naye Bwana akayaitikia maombo yake, ndipo, mkewe Rebeka alipopata mimba, 22Watoto walipogongana tumboni mwake, akasema: Kama ndivyo, nimevipatia nini? Akaenda kumwuliza Bwana. 23Bwana akamwambia:
Mataifa mawili yamo tumboni mwako,
kabila mbili za watu zinatengana tumboni mwako
zikitaka kutoka,
kabila moja itatenda nguvu kuishinda ile nyingine,
naye mkubwa atamtumikia nduguye.#1 Mose 27:29; Mal. 1:2; Rom. 9:10-12.
24Siku zake za kuzaa zilipotimia, ikaonekana, ya kuwa wana wa pacha wamo tumboni mwake. 25Wa kwanza alipotoka alikuwa mwekundu, mwenye manyoya mwilini mote kama vazi la ngozi, wakamwita jina lake Esau. 26Ndugu yake alipotoka baadaye, mkono wake ulikuwa unakishika kisigino cha Esau, wakamwita jina lake Yakobo. Naye Isaka alikuwa mwenye miaka 60, mkewe alipowazaa. 27Hawa watoto walipokua, Esau akawa wa porini na fundi wa kuwinda, lakini Yakobo akawa mtulivu, akapenda kukaa hemani. 28Kwa hiyo Isaka akampenda Esau, kwa kuwa alimpatia nyama za kula za porini, lakini Rebeka alikuwa anampenda Yakobo.
Esau anamwuzia Yakobo ukubwa wake.
29Siku moja Yakobo alipopika kunde, Esau akarudi toka porini, naye alikuwa amechoka sana. 30Ndipo, Esau alipomwambia Yakobo: Nipe, nile upesi hicho chekunduchekundu! Kwani nimechoka sana. Kwa sababu hii wakaliita jina lake Edomu (Mwekundu). 31Lakini Yakobo akasema: Niuzie leo hivi ukubwa wako! 32Naye Esau akasema: Tazama, mimi ninakwenda kufa! Hapo ukubwa utanifaa nini? 33Yakobo akasema: Uniapie leo hivi! Basi, akamwapia; hivyo ndivyo, alivyomwuzia Yakobo ukubwa wake.#1 Mose 27:36; Ebr. 12:16. 34Kisha Yakobo akampa mkate na hizo kunde, alizozipika; naye akala, akanywa, kisha akainuka, akaenda zake. Hivyo ndivyo, Esau alivyoubeza ukubwa.

Iliyochaguliwa sasa

1 Mose 25: SRB37

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia