1
1 Mose 25:23
Swahili Roehl Bible 1937
Bwana akamwambia: Mataifa mawili yamo tumboni mwako, kabila mbili za watu zinatengana tumboni mwako zikitaka kutoka, kabila moja itatenda nguvu kuishinda ile nyingine, naye mkubwa atamtumikia nduguye.
Linganisha
Chunguza 1 Mose 25:23
2
1 Mose 25:30
Ndipo, Esau alipomwambia Yakobo: Nipe, nile upesi hicho chekunduchekundu! Kwani nimechoka sana. Kwa sababu hii wakaliita jina lake Edomu (Mwekundu).
Chunguza 1 Mose 25:30
3
1 Mose 25:21
Isaka akamwombea mkewe kwake Bwana, kwani alikuwa mgumba; naye Bwana akayaitikia maombo yake, ndipo, mkewe Rebeka alipopata mimba
Chunguza 1 Mose 25:21
4
1 Mose 25:32-33
Naye Esau akasema: Tazama, mimi ninakwenda kufa! Hapo ukubwa utanifaa nini? Yakobo akasema: Uniapie leo hivi! Basi, akamwapia; hivyo ndivyo, alivyomwuzia Yakobo ukubwa wake.
Chunguza 1 Mose 25:32-33
5
1 Mose 25:26
Ndugu yake alipotoka baadaye, mkono wake ulikuwa unakishika kisigino cha Esau, wakamwita jina lake Yakobo. Naye Isaka alikuwa mwenye miaka 60, mkewe alipowazaa.
Chunguza 1 Mose 25:26
6
1 Mose 25:28
Kwa hiyo Isaka akampenda Esau, kwa kuwa alimpatia nyama za kula za porini, lakini Rebeka alikuwa anampenda Yakobo.
Chunguza 1 Mose 25:28
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video