Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Mose 29

29
Yakobo anamtumikia Labani.
1Kisha Yakobo akashika njia kwenda katika nchi yao wana wa upande wa maawioni kwa jua. 2Huko akaona kisima njiani, tena akaona makundi matatu ya mbuzi na kondoo waliopumzika hapo, kwani humo kisimani ndimo, walimonyweshea makundi yao, nalo jiwe lililowekwa juu mdomoni pa kisima lilikuwa kubwa. 3Huko ndiko, makundi yote yalikokusanyikia, kisha wakaliondoa hilo jiwe mdomoni pa kisima na kulifingirisha; tena walipokwisha kuyanywesha makundi yao, wakalirudisha mahali pake mdomoni pa kisima. 4Naye Yakobo akawauliza: Ndugu, mnatoka wapi? Wakasema: Tumetoka Harani. 5Akawauliza: Mwamjua Labani, mwana wa Nahori? Wakajibu: Twamjua. 6Akawauliza tena: Hajambo? Wakajibu: Hajambo, tena tazama! Mwanawe wa kike, Raheli, anakuja na kundi lake. 7Akasema: Tazameni, jua liko juu bado, saa za kukusanyikia makundi hazijatimia bado; wanywesheni mbuzi na kondoo, kisha walisheni! 8Wakajibu: Hatuwezi, mpaka makundi yote yakusanyike, wote waliondoe hili jiwe na kulifingirisha, tupate kuwanywesha mbuzi na kondoo.
9Angali akisema nao, Raheli akafika na kundi la baba yake, kwani alikua analichunga. 10Yakobo alipomwona Raheli, binti Labani aliyekuwa umbu la mama yake, nalo kundi la Labani aliyekuwa umbu la mama yake, Yakobo akafika karibu, akalifingirisha lile jiwe, liondoke mdomoni pa kisima, akawanywesha mbuzi na kondoo wa Labani aliyekuwa umbu la mama yake. 11Kisha Yakobo akamnonea Raheli, akaipaza sauti yake na kulia. 12Yakobo akamsimulia Raheli, ya kuwa yeye ni ndugu ya baba yake kwa kuwa mwana wa Rebeka; ndipo, alipopiga mbio kwenda kumpasha baba yake habari. 13Ikawa, Labani alipozisikia habari za Yakobo, mwana wa umbu lake, akamkimbilia, akamkumbatia na kumnonea, kisha akampeleka nyumbani mwake. Naye akamsimulia Labani hayo mambo yote ya kwao. 14Ndipo, Labani alipomwambia: Kweli wewe na mimi tu mfupa mmoja na nyama za mwili mmoja. Akakaa kwake siku kama za mwezi mmoja.
15Kisha Labani akamwambia Yakobo: Ijapo u ndugu yangu, kwa hiyo utanitumikia bure? Niambie mshahara wako, unaoutaka! 16Naye Labani alikuwa na wana wa kike wawili, mkubwa jina lake ni Lea, mdogo jina lake ni Raheli. 17Macho yake Lea yalikuwa yemepumbaapumbaa, lakini Raheli alikuwa mzuri wa umbo lake na wa uso wake. 18Kwa hiyo Yakobo akampenda Raheli, akasema: Nitakutumikia miaka saba, unipe mwanao mdogo Raheli. 19Labani akasema: Inafaa zaidi, nikupe wewe kuliko mtu mwingine; basi, kaa kwangu! 20Yakobo akamtumikia miaka saba, ampate Raheli, nayo ilikuwa machoni pake kama siku chache tu kwa kumpenda sana.
Ndoa ya Yakobo.
21Kisha Yakobo akamwambia Labani: Nipe mke wangu! Kwani siku zangu zimetimia, nipate kuingia kwake. 22Ndipo, Labani alipowakusanya watu wote wa mahali pale, akafanya karamu. 23Ilipokuwa jioni, akamchukua mwanawe Lea, akamwingiza kwake, naye akaingia kwake. 24Naye Labani akampa kijakazi wake Zilpa, amtumikie mwanawe Lea. 25Ilipokuwa asubuhi, Yakobo akaona, ya kama ndiye Lea; ndipo, alipomwuliza Labani: Mbona umenifanyizia hivyo? Sikukutumikia kumpata Raheli? Kwa nini umenidanganya? 26Labani akasema: Huku kwetu haiwezekani kumwoza mdogo, mkubwa wake akiwa hajaolewa. 27Maliza naye juma hili la ndoa, halafu tutakupa naye yule, ukinitumika tena miaka saba mingine. 28Yakobo akafanya hivyo, akalimaliza juma hilo la ndoa, kisha akampa naye mwanawe Raheli kuwa mkewe. 29Naye mwanawe Raheli Labani akampa kijakazi wake Biliha, amtumikie. 30Hivyo akapata kuingia hata kwake Raheli, akampenda kuliko Lea; kwa kumpata naye akamtumikia tena miaka saba mingine.#3 Mose 18:18.
Wana wa kwanza wa Lea.
31Bwana alipoona, ya kuwa Lea amechukiwa naye, akalifungua tumbo lake, lakini Raheli alikuwa mgumba. 32Ndipo, Lea alipopata mimba, akazaa mtoto mume, akamwita jina lake Rubeni (Tazameni Mtoto), kwani alisema: Bwana ameutazama ukiwa wangu; kwani sasa mume wangu atanipenda. 33Akapata mimba tena, akazaa mtoto mume, akasema: Kwa kuwa Bwana amesikia, ya kama nimechukiwa, amenipa huyu mtoto naye, kwa hiyo akamwita jina lake Simeoni (Kusikiwa). 34Akapata mimba tena, akazaa mtoto mume, akasema: Sasa mara hii mume wangu ataandamanishwa na mimi, kwa kuwa nimemzalia watoto waume watatu, kwa hiyo akamwita jina lake Lawi (Mwandamano). 35Akapata mimba tena, akazaa mtoto mume, akasema: Mara hii nitamshukuru Bwana, kwa hiyo akamwita jina lake Yuda (Shukrani). Kisha akakoma kuzaa.

Iliyochaguliwa sasa

1 Mose 29: SRB37

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia