Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Mose 37

37
Ndoto za Yosefu.
1Yakobo akakaa katika nchi hiyo, baba yake alikokaa ugenini, ndio nchi ya Kanaani. 2Hivi ni vizazi vya Yakobo: Yosefu alipopata miaka 17, akachunga mbuzi na kondoo pamoja na kaka zake; huyu kijana Yosefu alipokuwa pamoja na wana wa Biliha nao wana wa Zilpa, wakeze baba yake, yeye Yosefu akamsimulia baba yao mambo yao mabaya. 3Naye Isiraeli alimpenda Yosefu kuliko wanawe wote, kwa kuwa ni mwanawe wa uzee wake; kwa hiyo akamshonea kanzu ya nguo za rangi. 4Kaka zake walipoona, ya kuwa baba yao alimpenda kuliko ndugu zake, wakamchukia, hawakuweza kusema naye kwa upole.
5Kisha Yosefu akaota ndoto, akawasimulia kaka zake; ndipo, walipozidi kumchukia, 6kwani aliwaambia: Isikieni ndoto hii, niliyoiota! 7Nimeona, sisi tulikuwa shambani tukifunga miganda; mara mganda wangu ukainuka, ukasimama, nayo miganda yenu ikauzunguka, ikazungukia mganda wangu. 8Ndipo, kaka zake walipomwambia: Je? Unataka kuwa mfalme wetu, ututawwale? Wakazidi kumchukua sana kwa ajili ya ndoto zake na kwa ajili ya maneno yake. 9Akaota tena ndoto nyingine, akaisimulia nayo kaka zake akiwaambia: Tazameni! Nimeota ndoto nyingine, nikaona, jua na mwezi na nyota kumi na moja zikiniangukia. 10Alipomsimulia baba yake nao kaka zake ndoto hizi, baba yake akamkemea, akamwambia: Hiyo ndoto yako, uliyoiota, ni ndoto gani? Je? mimi na mama yako na kaka zako tuje, tukuangukie chini? 11Ndipo, kaka zake walipomwonea wivu, lakini baba yake akayashika maneno hayo na kuyaangalia.
Kuuzwa kwake Yosefu.
12Kisha kaka zake walipokwenda kuwachnga mbuzi na kondoo wa baba yao huko Sikemu,#1 Mose 33:18-19. 13Isiraeli akamwambia Yosefu: Kumbe kaka zako hawako Sikemu wakichunga mbuzi na kondoo? Haya! Nikutume kwenda kwao! Akamwitikia: Mimi tayari. 14Akamwambia: Nenda kuwatazama kaka zako, kama hawajambo, nao mbuzi na kondoo, kama hawajambo! Kisha uniletee habari! Akamtuma kutoka bondeni kwa Heburoni kwenda Sikemu.#1 Mose 35:27. 15Ndipo, mtu alipomwona, alipokuwa amepotelewa na njia porini, naye yule mtu akamwuliza: Unatafuta nini? 16Akasema: Ninawatafuta kaka zangu; niambie, wanakochungia mbuzi na kondoo! 17Yule mtu akasema: Wameondoka huku, kwani naliwasikia, wakisema: Na twende Dotani! Basi, Yosefu alipowafuata kaka zake akawaona Dotani. 18Nao walipomwona, angaliko mbali, wakafanya shauri la kumwua, alipokuwa hajafika kwao, 19wakasemezana: Mtazameni Chandoto! Huyu, anakuja! 20Sasa haya! na tumwue! Kisha tumtupe shimoni mo mote, tuseme: Nyama mkali amemla! Ndipo, tutakapoona, ndoto zake zitakavyotimia. 21Rubeni alipoyasikia alitaka kumponya mikononi mwao, akawaambia: Tusimwue!#1 Mose 42:22. 22Kisha Rubeni akawaambia: Msimwage damu yake! Mtupeni humu shimoni huku nyikani! Lakini msimwue kwa kumpelekea mikono! Naye alisema hivyo, apate kumponya mikononi mwao, amrudishe kwa baba yake.
23Ikawa, Yosefu alipofika kwa kaka zake, wakamvua kanzu yake, maana aliivaa ile kanzu ya nguo za rangi;#1 Mose 37:3. 24kisha wakamchukua, wakamtumbukiza katika shimo, nalo hilo shimo lilikuwa halina maji.#Yer. 38:6. 25Kisha wakakaa, wale chakula. Walipoyainua macho yao kutazama, mara wakaona msafara wa Waisimaeli waliotoka Gileadi wenye ngamia waliochukua manukato na mafuta ya mkwaju na uvumba, nao walikwenda kuvipeleka Misri. 26Ndipo, Yuda alipowaambia ndugu zake: Haifai, tukimwua ndugu yetu na kuificha damu yake; 27haya! na tumwuze kwa hawa Waisimaeli, tusimpige kwa mikono yetu! Kwani ni ndugu yetu, tuliyezaliwa naye. Nao ndugu zake wakamwitikia. 28Basi, hao wachuuzi wa Midiani walipopita, wakamwopoa Yosefu na kumtoa mle shimoni, wakamwuza Yosefu kwao hao Waisimaeli kwa fedha 20, nao wakampeleka Yosefu Misri.#1 Mose 25:2.
29Rubeni aliporudi hapo shimoni, akaona, ya kama Yosefu hayumo; ndipo, alipozirarua nguo zake,#1 Mose 44:13; 2 Sam. 1:11. 30akarudi kwa ndugu zake, akawaambia: Mtoto hayumo, mimi nami niende wapi?
Kusikitika kwake Yakobo.
31Kisha wakaichukua kanzu ya Yosefu, wakachinja dume la mbuzi, wakaichovya hiyo kanzu katika damu yake. 32Kisha wakaituma hiyo kanzu ya nguo za rangi kumpelekea baba yao, wakamwambia: Nguo hii tumeiokota; itazame, kama ndiyo kanzu ya mwanao, au kama siyo! 33Akaitambua, akasema: Ni kanzu ya mwanangu! Nyama mkali amemla, Yosefu ameraruliwa kweli!#1 Mose 37:20. 34Ndipo, Yakobo alipozirarua nguo zake, akavaa gunia kiunoni, akamwombolezea mwanawe siku nyingi.#1 Mose 37:29. 35Wakainuka wanawe wote wa kiume nao wote wa kike, wamtulize moyo, lakini akakataa kutulizwa moyo akisema: Nitashuka mwenye ukiwa huko kuzimuni, mwanangu aliko. Ndivyo, baba yake alivyomlilia.
36Wale Wamidiani wakamwuza huko Misri kwa Potifari aliyekuwa mtumishi wa nyumbani mwa Farao na mkuu wao waliomlinda Farao.

Iliyochaguliwa sasa

1 Mose 37: SRB37

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia