1
1 Mose 37:5
Swahili Roehl Bible 1937
Kisha Yosefu akaota ndoto, akawasimulia kaka zake; ndipo, walipozidi kumchukia
Linganisha
Chunguza 1 Mose 37:5
2
1 Mose 37:3
Naye Isiraeli alimpenda Yosefu kuliko wanawe wote, kwa kuwa ni mwanawe wa uzee wake; kwa hiyo akamshonea kanzu ya nguo za rangi.
Chunguza 1 Mose 37:3
3
1 Mose 37:4
Kaka zake walipoona, ya kuwa baba yao alimpenda kuliko ndugu zake, wakamchukia, hawakuweza kusema naye kwa upole.
Chunguza 1 Mose 37:4
4
1 Mose 37:9
Akaota tena ndoto nyingine, akaisimulia nayo kaka zake akiwaambia: Tazameni! Nimeota ndoto nyingine, nikaona, jua na mwezi na nyota kumi na moja zikiniangukia.
Chunguza 1 Mose 37:9
5
1 Mose 37:11
Ndipo, kaka zake walipomwonea wivu, lakini baba yake akayashika maneno hayo na kuyaangalia.
Chunguza 1 Mose 37:11
6
1 Mose 37:6-7
kwani aliwaambia: Isikieni ndoto hii, niliyoiota! Nimeona, sisi tulikuwa shambani tukifunga miganda; mara mganda wangu ukainuka, ukasimama, nayo miganda yenu ikauzunguka, ikazungukia mganda wangu.
Chunguza 1 Mose 37:6-7
7
1 Mose 37:20
Sasa haya! na tumwue! Kisha tumtupe shimoni mo mote, tuseme: Nyama mkali amemla! Ndipo, tutakapoona, ndoto zake zitakavyotimia.
Chunguza 1 Mose 37:20
8
1 Mose 37:28
Basi, hao wachuuzi wa Midiani walipopita, wakamwopoa Yosefu na kumtoa mle shimoni, wakamwuza Yosefu kwao hao Waisimaeli kwa fedha 20, nao wakampeleka Yosefu Misri.
Chunguza 1 Mose 37:28
9
1 Mose 37:19
wakasemezana: Mtazameni Chandoto! Huyu, anakuja!
Chunguza 1 Mose 37:19
10
1 Mose 37:18
Nao walipomwona, angaliko mbali, wakafanya shauri la kumwua, alipokuwa hajafika kwao
Chunguza 1 Mose 37:18
11
1 Mose 37:22
Kisha Rubeni akawaambia: Msimwage damu yake! Mtupeni humu shimoni huku nyikani! Lakini msimwue kwa kumpelekea mikono! Naye alisema hivyo, apate kumponya mikononi mwao, amrudishe kwa baba yake.
Chunguza 1 Mose 37:22
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video