Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Mose 38

38
Kosa baya la Yuda.
1Ikawa wakati huo, ndipo, Yuda alipoondoka kwa ndugu zake, akajiunga na mtu wa Adulamu, jina lake Hira. 2Huko Yuda akaona binti Mkanaani, jina lake sua, akamchukua, akaingia kwake. 3Naye akapata mimba, akazaa mtoto mume; jina lake yule akamwita Eri. 4Alipopata mimba tena akazaa mtoto mume, akamwita jina lake Onani. 5Akendelea, akazaa tena mtoto mume, akamwita jina lake Sela. Naye Yuda alikuwa huko Kizibu, alipomzaa.
6Yuda akamwoza mwanawe wa kwanza Eri, jina lake mkewe ni Tamari. 7Lakini Eri, mwana wa kwanza wa Yuda, akawa mbaya machoni pa Bwana, kwa hiyo Bwana akamwua. 8Ndipo, Yuda alipomwambia Onani: Ingia kwa mkewe kaka yako, umsimikie unyumba naye na kumpatia kaka yako mzao kwake!#5 Mose 25:5. 9Kwa kuwa Onani alijua, ya kama huyo mzao hatakuwa wake yeye, basi, kila mara alipoingia kwa mkewe kaka yake kwanza akaziangusha mbegu zake chini, asimpatie kaka yake uzao. 10Hayo, aliyoyafanya, yakawa mabaya machoni pa Bwana, kwa hiyo akamwua naye. 11Ndipo, Yuda alipomwambia mkwewe Tamari: Kaa tu na ujane wako nyumbani mwa baba yako, hata mwanangu Sela akue! Kwani alisema moyoni, asife huyu naye kama kaka zake. Kwa hiyo Tamari akaenda, akakaa nyumbani mwa baba yake.
12Siku zilipopita nyingi, binti Sua, mkewe Yuda, akafa. Yuda alipokwisha kujituliza moyo kwa ajili ya kufa kwake akapanda kwenda Timunati kwao waliowakata kondoo wake manyoya, yeye na rafiki yake Hira wa Adulamu. 13Tamari alipopashwa habari kwamba: Tazama, mkweo anapanda kwenda Timunati kuwakata kondoo wake manyoya, 14akayavua mavazi yake ya ujane, akajifunika kwa ukaya na kujitandia nguo, kisha akakaa hapo pa kuingilia Enaimu kwenye njia ya timunati, kwani aliona, ya kuwa Sela amekwisha kukua, lakini yeye hakuozwa naye, awe mkewe. 15Yuda alipomwona akamwazia kuwa mwanamke mgoni, kwani alijifunika ushungi, 16akamgeukia na kumwendea hapo njiani, alipokaa, akamwambia: Acha, niingie kwako! kwani hakumjua kuwa mkwewe. Akamwuliza: Utanipa nini ukiingia kwangu?#3 Mose 18:15. 17Akasema: Mimi nitakuletea dume la mbuzi, nitakayemtoa mle makundini; naye akamwambia: Nipe rehani, niishike, mpaka utakapomleta! 18Akamwuliza: Nikupe rehani gani? Akamwambia: Pete yako yenye muhuri na mshipi wako na fimbo yako, unayoishika mkononi. Akampa, kisha akaingia kwake, naye akapata mimba. 19Alipoinuka kwenda zake, akaondoa ukaya wake usoni pake, akayavaa mavazi yake ya ujane. 20Yuda alipotuma dume la mbuzi mkononi mwa rafiki yake wa Adulamu, achukue nazo zile rehani mkononi mwa yule mwanamke, hakumwona. 21Naye alipowauliza watu wa mahali hapo kwamba: Yuko wapi yule mwanamke mgoni wa patakatifu aliyekaa njiani hapo Enaimu? Wakamwambia: Huku hakuwako mwanamke mgoni wa patakatifu. 22Akarudi kwake Yuda, akamwambia: sikumwona, nao watu wa mahali pale wanasema: Huku hakuwako mwanamke mgoni wa patakatifu. 23Ndipo, Yuda aliposema: Na ajitwalie, tusije kutwezwa! Tazama, nimempeleka huyu dume la mbuzi, nawe hukumwona!
24Miezi mitatu ilipopita, Yuda akapashwa habari kwamba: Mkweo Tamari amefanya ugoni, naye akapata mimba kwa huo ugoni. Ndipo, Yuda aliposema: Mtoeni, ateketezwe! 25Alipotolewwa akatuma kwa mkwewe kwamba: Mimi nimepata mimba kwake yeye aliye mwenye vitu hivi; akaendelea kusema: Mtambue mwenye pete hii yenye muhuri na mwenye mshipi huu na mwenye fimbo hii! 26Yuda alipovitambua vitu hivyo akasema: Yeye ni mwongofu kuliko mimi; ameyafanya, kwa kuwa sikumpa mwanangu Sela. Lakini hakumjua tena hata mara moja.
27Siku zake za kuzaa zilipotimia, wakaona ya kuwa tumboni mwake wamo wana wa pacha. 28Ikawa, alipozaa, mmoja akatoa mkono; ndipo mzalishaji alipomfunga mkononi pake uzi mwekundu kwamba: Huyu ametoka wa kwanza. 29Lakini ikawa, alipourudisha mkono wake, mara ndugu yake akatoka; ndipo, aliposema: Kumbe umejipasulia ufa namna hii! Kwa hiyo wakamwita jina lake Peresi (Ufa). 30Kisha ndugu yake akatoka naye mwenye uzi mwekundu mkononi pake, kwa hiyo wakamwita jina lake Zera (Mwekundu).

Iliyochaguliwa sasa

1 Mose 38: SRB37

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia