Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Mose 39

39
Yosefu anamtumikia Potifari.
1Yosefu alipopelekwa Misri, Potifari aliyekuwa mtumishi wa nyumbani mwa Farao na mkuu wao waliomlinda Farao akamnunua mikononi mwao wale Waisimaeli waliompeleka huko.#1 Mose 37:28. 2Bwana akawa naye Yosefu, kwa hiyo akafanikiwa alipokuwa nyumbani mwa bwana wake wa Kimisri. 3Bwana wake alipoona, ya kuwa Bwana yuko pamoja naye, nayo yote, anayoyafanya, Bwana anayafanikisha mikononi mwake, 4Yosefu akaona upendeleo machoni pake, akampa kumtumikia mwenyewe, kisha akamweka kuisimamia nyumba yake yote, nayo yote, aliyokuwa nayo, akayatia mkononi mwake. 5Tangu hapo, alipomweka nyumbani mwake kuyasimamia yote, aliyokuwa nayo, Bwana akaibariki nyumba ya huyu Mmisri kwa ajili yake Yosefu; mbaraka ya Bwana ikayakalia yote yaliyokuwa yake nyumbani na shambani.#1 Mose 30:27. 6Kwa hiyo akamwachia Yosefu yote, aliyokuwa nayo, yawe mkononi mwake, naye mwenyewe hakujua chake cho chote, isipokuwa chakula chake, alichokila.
Yosefu anamkataa mkewe Potifari.
Naye Yosefu alikuwa mzuri wa umbo na wa uso. 7Siku zilipopita, mkewe bwana wake akamtupia Yosefu macho, akamwambia: Lala kwangu!#Fano. 5:3. 8Lakini akakataa, akamwambia mkewe bwana wake: Tazama! Bwana wangu hajui cho chote kilichomo humu nyumbani, ninachokiangalia, nayo yote, aliyo nayo, ameyatia mkononi mwangu. 9Humu nyumbani hamna mkubwa kuliko mimi, wala hamna kitu, alichonikataza, ni wewe peke yako, kwa kuwa wewe ndiwe mkewe. Kwa hiyo nitawezaje kufanya kibaya kilicho kikuu kama hiki nikimkosea Mungu?#2 Mose 20:14. 10Hivi ndivyo, alivyomwambia Yosefu siku kwa siku, lakini Yosefu hakumwitikia kulala naye wala kuwa pamoja naye.
11Ikawa siku moja, alipoingia kufanya kazi zake chumbani, msimokuwa na mtu hata mmoja wao wakazi wa humo chumbani, 12ndipo, alipomkamata nguo yake na kusema: Lala kwangu! Lakini akaiacha nguo yake mkononi mwake, akakimbia na kutoka nje. 13Ikawa, alipoona, ya kuwa ameiacha nguo yake mkononi mwake na kukimbia kwenda nje, 14akawaita waliomo nyumbani, akawaambia kwamba: Tazameni! Ametuletea huyu Mwebureo wa kucheza na sisi! Ameingia mwangu kulala na mimi, lakini nikapiga kelele kubwa. 15Naye aliposikia, ya kama nimezipaza sauti zangu za kuita watu, akaiacha nguo yake kwangu, akakimbia kwenda nje. 16Akaiweka nguo yake kwake, hata bwana wake arudi nyumbani mwake. 17Ndipo, alipomwambia maneno yayo hayo ya kwamba: Yule mtumwa Mwebureo, uliyemleta kwetu kucheza na sisi, ameingia mwangu. 18Lakini nilipozipaza sauti zangu za kuita watu, akaiacha nguo yake kwangu, akakimbia kwenda nje.
Yosefu anafungwa.
19Ikawa, bwana wake alipoyasikia haya maneno ya mkewe, aliyomwambia ya kwamba: Mtumwa wako amenifanyia haya na haya, akakasirika na kuwaka moto. 20Ndipo, bwana wake Yosefu alipomchukua, akamfunga kifungoni mle chumbani, mlimokuwa na wafungwa wa mfalme; humo kifungoni ndimo, Yosefu alimotiwa. 21Lakini Bwana alikuwa naye Yosefu, akamtolea utu na kumpatia upendeleo machoni pa mkuu wa kifungo. 22Huyu mkuu wa kifungo akatia mkononi mwa Yosefu wafungwa wote waliokuwamo mle kifungoni, yote waliyoyafanya humo yawe kazi yake yeye. 23Katika yote, mkuu a kifungo aliyoyatia mkononi mwake, hakikuwamo cho chote, alichokitazama mwenyewe, kwa kuwa Bwana alikuwa na Yosefu, nayo yote aliyoyafanya Bwana akayafanikisha.

Iliyochaguliwa sasa

1 Mose 39: SRB37

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia