1 Mose 40
40
Yosefu anafumbua ndoto za wafungwa.
1Ikawa, mambo hayo yalipomalizika, mkuu wa watunza vinywaji vya mfalme wa Misri na mkuu wa wachoma mikate wakamkosea bwana wao, mfalme wa Misri. 2Naye Farao akawakasirikia hawa watumishi wake wawili wa nyumbani mwake, Yule mkuu wa watunza vinywaji naye mkuu wa wachoma mikate. 3Akawafunga, waangaliwe kifungoni katika nyumba ya mkuu wao waliomlinda mfalme; ndimo, Yosefu alimokuwa naye kwa kufungwa.#1 Mose 39:20. 4Naye mkuu wao waliomlinda mfalme akamweka Yosefu kuwaangalia na kuwatumikia, wakawamo hizo siku wakiangaliwa.
5Usiku mmoja wote wawili wakaota ndoto, kila mtu ndoto yake yenye maana yake, yule mtunza vinywaji vya mfalme naye yule mchoma mikate ya mfalme wa Misri waliokuwa wamefungwa kifungoni. 6Yosefu alipoingia asubuhi chumbani mwao, awatazame, akawaona, ya kuwa wamenuna, 7akawauliza hawa wafungwa wa Farao walioangaliwa naye katika nyumba ya bwana wake kwamba: Mbona leo nyuso zenu ni mbaya? 8Wakamwambia: Tumeota ndoto, lakini mwenye kuzifumbua hakuna. Yosefu akawaambia: Kumbe kufumbua siko kwake Mungu? Lakini nisumulieni! 9Mkuu wao watunza vinywaji akamsimulia ndoto yake, akamwambia: Katika ndoto yangu nimeona machoni pangu mzabibu; 10katika mzabibu huu yalikuwamo matawi matatu, nao ulipochipuka, ukachanua maua yake, navyo vichala vyake vikaivisha zabibu. 11Nacho kikombe cha Farao kilikuwa mkononi mwangu, nikazishika zile zabibu, nikazikamulia katika kikombe cha Farao, kisha nikampa Farao, hicho kikombe mkononi mwake. 12Yosefu akamwambia: Maana yake ndio hii: hayo matawi matatu ndio siku tatu; 13siku tatu zitakapopita, Farao atakupa kukiinua kichwa chako, kwani atakurudisha katika kazi yako, umpe kikombe chake Farao mkononi mwake, kama ilivyokupasa kale, ulipokuwa mtunza vinywaji vyake. 14Lakini utakapopata mema sharti unikumbe na kunihurumia ukiniombea kwake Farao, anitoe humu nyumbani. 15Kwani nimekwibwa katika nchi ya Waebureo, huku nako sikukosa lo lote, wakanitia humu kifungoni.#1 Mose 37:28.
16Mkuu wa wachoma mikate alipoona, ya kuwa amefumbua vema, akamwambia Yosefu: Mimi nami katika ndoto yangu nimejiona, nilipokuwa nimechukua nyungo tatu zenye vikate vyeupe kichwani pangu. 17Namo katika ungo wa juu vilikuwamo vikate vizuri vyo vyote vya Farao, wachoma mikate wanavyovitengeneza, nao ndege wakavila mwenye ungo kichwani pangu. 18Yosefu akajibu akisema: Maana yake ndio hii: hizo nyungo tatu ndio siku tatu; 19siku tatu zitakapopita, Farao atakupa kukiinua kichwa chako, kiwe juu yako zaidi, atakunyonga katika mti, nao ndege watazila nyama za mwili wako.
Ndoto zao wale wafungwa zinatimia, kama Yosefu alivyosema.
20Siku ya tatu ikawa siku ya kuzaliwa kwake Farao; ndipo, alipowaandalia watumishi wake wote karamu; hapo katikati ya watumishi wake akampa mkuu wa watunza vinywaji naye mkuu wa wachoma mikate kuviinua vichwa vyao, 21akimrudisha mkuu wa watunza vinywaji katika kazi yake ya kutunza vinywaji, ampe Farao kikombe mkononi mwake, 22naye mkuu wa wachoma mikate akamnyonga, kama Yosefu alivyowafumbulia ndoto. 23Lakini mkuu wa watunza vinywaji hakumkumbuka Yosefu, akamsahau.#1 Mose 40:14.
Iliyochaguliwa sasa
1 Mose 40: SRB37
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.