Mwanzo 39:20-21
Mwanzo 39:20-21 NMM
Potifa akamchukua Yusufu na kumweka gerezani, mahali ambapo wahalifu wa mfalme walikuwa wamefungwa. Lakini wakati Yusufu alipokuwa huko gerezani, BWANA alikuwa pamoja naye, akamhurumia na kumpa kibali mbele ya msimamizi wa gereza.