Methali 24:7-12
Methali 24:7-12 BHN
Kwa mpumbavu hekima ni ngumu kuielewa; penye mkutano wa mashauri hafungui mdomo. Afikiriaye kutenda maovu daima ataitwa mtu mwenye fitina. Mpango anaofikiria mpumbavu ni dhambi; mwenye dharau huchukiwa na kila mtu. Ukifa moyo wakati wa shida, basi wewe ni dhaifu kweli. Mwokoe mtu anayechukuliwa kuuawa bure; usisite kumwokoa anayeuawa bila hatia. Usiseme baadaye: “Hatukujua!” Maana Mungu apimaye mioyo ya watu huona; yeye atakulipa kulingana na matendo yako!