Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ahadi za kila siku ya maisha yakoMfano

Ahadi za kila siku ya maisha yako

SIKU 28 YA 30

Mungu ananena na wewe

Inaonekana kama jambo kawaida na   la kimsingi, lakini naamini kuna wengi ambao bado wanajiuliza kama Mungu   anazungumza kweli na watu. Umewahi kujiuliza kuhusu hili? Je! Unajiuliza kama   Mungu atawahi kuzungumza na wewe? Utakuwa na furaha kujua kwamba jibu ni   ndiyo.

Kufikia mwisho   wa wakati wake duniani, Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Hata   bado nikali ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili hivi   sasa.
Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli,   atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake ( Yohana 16:12-13)

Yesu alipokuwa   akisema maneno haya, alikuwa anaongea na watu ambao alikuwa ametumia miaka   mitatu nao ... bado alikuwa na zaidi ya kuwafundisha. Hii ni ya kushangaza,   kwa sababu ningefikiri kwamba ikiwa Yesu alikuwa na mimi binafsi kwa miaka   mitatu, mchana na usiku, ningekuwa nimejifunza kila kitu ambacho ni lazima nijue.
Lakini Yesu daima ana mengi ya   kusema kwa sababu tutakuwa daima tunakabiliwa na hali mpya katika maisha   ambayo anataka kutuongoza. Ndiyo maana tumepewa Roho Mtakatifu-ili tuweze kumsikia   Mungu akinena, ingawa Yeye hawezi kuwa kimwili mbele yetu

Kupitia   Kristo, na nguvu za Roho Mtakatifu, Mungu anataka kuzungumza na wewe ana kwa   ana kwa kila siku. Anataka kukuongoza hatua kwa hatua kwa vitu vyema ambavyo   amekuhifadhia.

Baba atatoa   zawadi ya Roho Wake kwa wote wanaomuomba (angalia Luka 11:13). Ninataka tena   kusema kwa uwazi kwamba kila mmoja wetu anaweza kusikia kutoka kwa Mungu na   kuongozwa na Roho Mtakatifu kila siku. Je! Unasikiliza?

OMBI LA KUANZA SIKU

 Mungu, naomba kuongozwa na Roho   Mtakatifu. Ninaamini kwamba Wewe unaongea na mimi, na ninataka kujua ni nini unasema.

Andiko

siku 27siku 29

Kuhusu Mpango huu

Ahadi za kila siku ya maisha yako

Mungu ametupa ahadi tele ambazo tunahitaji kutembea ndani yake. Lakini ni muhimu kuzijua, kuziamini ili tuweze kuziona zikidhirika maishani mwetu. Kila siku, kuna ahadi kwa ajili yako. Unapoanza siku yako, pata kufahamu ahadi hizi! 

More

Tunataka kushukuru Joyce Meyer Ministries kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: tv.joycemeyer.org/kiswahili