Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ahadi za kila siku ya maisha yakoMfano

Ahadi za kila siku ya maisha yako

SIKU 1 YA 30

 Jinsi ya kudumu katika uwepo wake kila siku 

Maisha yetu yana shughuli   nyingi na vizuizi vingi.Ni rahisi sana kushikika katika shughuli, wasiwasi na   majukumu hadi tukasahau kile kilicho cha muhimu zaidi.

Kuna hadithi fupi ya kupendeza   mwishoni mwa Luka 2 wakati Maria na Yusufu walimpeleka Yesu Yerusalemu kwa   pasaka akiwa umri wa miaka 12. Baada ya sherehe walianza safari kurudi   nyumbani wakidhani kwamba yuko nao.

Nami najiuliza, ni mara ngapi   tunadhani Mungu yuko nasi ilhali tumeenenda katika shughuli zetu wenyewe.

Sasa jambo la kushangaza ni   hili; Maria na Yusufu walikuwa wamesafiri siku nzima kutambua kuwa Yesu   hakuwa nao na iliwachukua siku tatu kumpata. Siku tatu! Sasa ujumbe hapa ni   huu; ni rahisi sana kwetu kuupoteza uwepo spesheli wa Mungu kuliko kuupata   tena tunapoupoteza.

Inafaa tuwe waangalifu kusalia   katika uwepo wa Mungu. Tunapofanya hivyo, Mungu hupata maskani mioyoni mwetu.

Hii huanza kwa kuwa watiifu kwa   neno la Mungu. Njia moja ya kuonyesha ukomavu wa kiroho ni kuachana na tabia   ambazo hazimpendezi Mungu, hii huonyesha kwamba unayajali yale anayofikiria.

Hii inamaanisha unakuwa mkarimu   kwa watu, unajifundisha kusamehe, unaachana na migogoro na unaishi kwa amani.   Tunapojifunza kuwa makini na maneno yaetu, kumshukuru Mungu na kuwainua   wengine, tutazidi kuwa katika uwepo wa Mungu siku nzima.

OMBI LA KUANZA SIKU

Baba, asante kwa kufanya moyo wangu   makao yako. Ninahitaji uwepo wako leo. Nisaidie nikuheshimu kwa mawazo na   maneno yangu, na kuwa wa Baraka kwa wale walio karibu name.

Andiko

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Ahadi za kila siku ya maisha yako

Mungu ametupa ahadi tele ambazo tunahitaji kutembea ndani yake. Lakini ni muhimu kuzijua, kuziamini ili tuweze kuziona zikidhirika maishani mwetu. Kila siku, kuna ahadi kwa ajili yako. Unapoanza siku yako, pata kufahamu ahadi hizi! 

More

Tunataka kushukuru Joyce Meyer Ministries kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: tv.joycemeyer.org/kiswahili

Mipango inayo husiana