Ahadi za kila siku ya maisha yakoMfano
Neema, nguvu ya Mungu ilyopeanwa bure
Ikiwa umeishi ulimwenguni humu kwa muda, utakubaliana name kwmba mara nyingi, mambo hayaendi jinsi ungetaka. Tunashukuru kwamba Mungu kamwe hataturuhusu katika hali yoyote ile bila kutupa uwezo wa kufurahi katika hali hiyo.
Ninaamini Mungu anatupa neema yake maalum kwa kila hali. Hivi ndivyo ninavyopenda kufafanua neema: "Nguvu ya Mungu kutusaidia kufanya chochote tunachohitaji kufanya." Unaweza kuwa na nguvu hiyo leo, lakini unapaswa kuipokea, na njia pekee ya kuipokea ni kwa imani.
Warumi 12: 3 inasema kwamba Mungu amemgawia kila mtu kiasi cha imani
Jiulize leo, Ninafanya nini na imani yangu? Unaweka imani yako ndani yako mwenyewe, au kwa wengine, au kwa hali yako?
Hiyo sio kuishi katika neema, hiyo ni kuishi tu kwa nguvu zako mwenyewe na kazi zako. Na njia hiyo haiwezi kupata kazi kutendeka.
Lakini unapoachilia imani yako na kumtumaini Mungu kufanya kile ambacho huwezi kufanya, unaweka imani yako ndani yake
Kisha neema-nguvu za Mungu-zitakuja kupitia njia ya imani na itakuwezesha kufanya mambo ambayo yatakushangaza wewe na wengine.
Hapa ni ufafanuzi wangu wa neema tena: "Ni nguvu ya Mungu inayokuja kwetu bila malipo-maana haitugharimu chochote isipokuwa tu kuweka imani yetu kwa Mungu-kutuwezesha kufanya kwa urahisi kile ambacho hatuwezi kufanya kwa wenyewe na kiasi chochote ya mapambano au jitihada. "
Weka imani yako kwa Mungu. Anataka kukupa neema Yake leo.
OMBI LA KUANZA SIKU
Mungu, najua kwamba maisha hayataenda kila namna nitakavyotaka, lakini ninakuamini. Kwa imani, napokea neema yako-nguvu uliyopewa kwa uhuru kunisaidia kutembea kupitia hali yoyote niliyo nayo leo
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Mungu ametupa ahadi tele ambazo tunahitaji kutembea ndani yake. Lakini ni muhimu kuzijua, kuziamini ili tuweze kuziona zikidhirika maishani mwetu. Kila siku, kuna ahadi kwa ajili yako. Unapoanza siku yako, pata kufahamu ahadi hizi!
More
Tunataka kushukuru Joyce Meyer Ministries kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: tv.joycemeyer.org/kiswahili