Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ahadi za kila siku ya maisha yakoMfano

Ahadi za kila siku ya maisha yako

SIKU 30 YA 30

Mungu ataongoza safari yako 

Maisha ya Kikristo yanaweza   kulinganishwa na safari. Roho Mtakatifu ndiye kiongozi wetu ... Anatuongoza   kila siku. Na Yeye daima anatuongoza katika kile kinachofaa kwa maisha yetu.   Funguo la safari ya mafanikio na ya kufurahisha ni kumfuata.
Lakini kumfuata Mungu   kunamaanisha nini? Kimsingi, inamaanisha kumtii, kufuata uongozi wake, na   kufanya kile anachosema
Mara nyingi tunakimbia mbele ya   Mungu. Tunaweza kufikiria tunajua mwelekeo bora wa kuchukua au tunakosa uvumilivu   kwa muda wake na kuchukua hatua mbaya kwa vile inakaa ya haraka. Tatizo ni,   tukigundua kuwa barabara hiyo inaongoza kwenye mwisho wa wafu, tutapaswa   kurudi tena mahali ambapo tuliondoka kwenye njia mwafaka.
Habari njema ni, Mungu yuko   pale, akisubiri kutuongoza tena na kutuonyesha njia sahihi ya kwenda.
Bwana amepanga vizuri safari ya   kila mmoja. Tunahitaji kuelewa kikamilifu kwamba anatupenda, kwamba ni mwema   na mwenye haki na tunaweza kumwamini
Tunaweza kumtegemea Yeye   kutuongoza katika mwelekeo unaofaa kwetu. Tunaweza kumtegemea Yeye   kutusahihisha tunapopotea na kutuongoza kwenye mahali pa haki. Tunaweza   kumwamini yeye na wengine juu ya njia yetu. Tunaweza kumwamini Yeye kwa   maisha yetu ... tosha!
Fuata mwongozo wa Roho   Mtakatifu, kwa sababu Yeye anajua njia na atakuwa daima na wewe. Mwamini Yeye   kukuongoza katika mema yote aliyopanga kwa ajili yako muda mrefu kabla   hujazaliwa. Na ufurahie safari.

OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, Neno   lako linasema kwamba Wewe huelekeza hatua za waumini. Ninaamini wewe   unaniongoza kwenye safari uliyonayo kwa ajili yangu, na najua kwamba   nitakapotoka kwenye njia, utakuwa daima nami kunisaidia kurudi na kuendelea.

Andiko

siku 29

Kuhusu Mpango huu

Ahadi za kila siku ya maisha yako

Mungu ametupa ahadi tele ambazo tunahitaji kutembea ndani yake. Lakini ni muhimu kuzijua, kuziamini ili tuweze kuziona zikidhirika maishani mwetu. Kila siku, kuna ahadi kwa ajili yako. Unapoanza siku yako, pata kufahamu ahadi hizi! 

More

Tunataka kushukuru Joyce Meyer Ministries kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: tv.joycemeyer.org/kiswahili