Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ahadi za kila siku ya maisha yakoMfano

Ahadi za kila siku ya maisha yako

SIKU 22 YA 30

Kulalamika ni dhambi!


Katika Waefeso 4:29, mtume Paulo   anatuamuru tusitumie lugha yoyote isiyofaa au ya uchafu. Wakati mmoja,   sikujua kwamba hii ilikuwa ni pamoja na kulalamika, lakini tangu hapo   nilijifunza kwamba kunung'unika na kulalamika hunajisi maisha yetu
Ukweli ni huu, kulalamika ni   dhambi! Inasababishia watu matatizo mengi na huharibu furaha ya mtu yeyote   anayesikiliza.

Tunahitaji   kujiuliza, jinsi tunavyokuwa naharaka kukosa subira na kuanza kulalamika   tunapokamatwa katika msongamano wa magari au wakati tunasubiri kwenye njia za   kusafiri katika maduka ya vyakula au maduka yoyote yale? Je! Ni haraka gani   tunaweza kuona na kuelezea makosa yote ya marafiki zetu au wa familia? Je!   Tunalalamika juu ya kazi yetu wakati tunapaswa kumshukuru Mungu kwamba tuna   moja?
Dawa bora kwa kulalamika ni   shukrani. Watu wenye shukrani hawawezi kulalamika. Wanashugulika sana   kushukuru kwa vitu vyote vizuri hadi hawana muda wa kutambua mambo ambayo   wanaweza kulalamikia.
Biblia inasema kwamba tunapaswa   kuingia katika malango ya Mungu kwa sifa na shukrani. Wewe na mimi tunahitaji   kuifanya kuwa lengo la kila siku la kuishi maisha ya shukrani. Hebu kuwa na   mtazamo chanya na shukrani iwezekanavyo.

Jaribu kulala   usiku ukifikiri kila kitu unachopaswa kushukuru. Hebu liwe jambo la kwanza   unalotenda asubuhi. Shukuru Mungu kwa vitu "vidogo" au vitu ambavyo   unaweza kuchukulia kama kawaida: nafasi ya kuegesha gari, kuamka wakati wa   kazi, chakula, familia yako ... Usivunjike moyo wakati   unashindwa, lakini usikate tama na kuachana na mambo. Endelea mpaka   utengeneze tabia mpya na wewe unaishi na mtazamo wa shukrani.

Kuwa na   ukarimu na shukrani yako. Itaboresha uhusiano wako na Bwana.

OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, nataka   kuishi na mtazamo wa shukrani, kuanzia hivi sasa! Ninakushukuru sana kwa   kunipenda na kunipa baraka. Nisaidie kuona mambo mazuri ya maisha ili nipate   kushukuru.

Andiko

siku 21siku 23

Kuhusu Mpango huu

Ahadi za kila siku ya maisha yako

Mungu ametupa ahadi tele ambazo tunahitaji kutembea ndani yake. Lakini ni muhimu kuzijua, kuziamini ili tuweze kuziona zikidhirika maishani mwetu. Kila siku, kuna ahadi kwa ajili yako. Unapoanza siku yako, pata kufahamu ahadi hizi! 

More

Tunataka kushukuru Joyce Meyer Ministries kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: tv.joycemeyer.org/kiswahili