Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ahadi za kila siku ya maisha yakoMfano

Ahadi za kila siku ya maisha yako

SIKU 23 YA 30

Mungu hufanya kazi kupitia watu 


Asubuhi moja nilikuwa na wakati   wangu wa utulivu peke yangu na Mungu, na nikamwambia Bwana, "Je!   Unawezaje kusimama kuona watoto wako wote wanaopata maumivu, biashara haramu   ya kibinadamu, mauaji ya kijumla, udhalimu, uharibifu, umasikini duniani na   hufanyi kitu ? "

Sikuwa nasema   kama malalamiko au kwa sababu nilikuwa nikihoji uaminifu wake, na sijui hata   kama nilikuwa nikitarajia kupata jibu, lakini nilimuuliza tu. Mara jibu lake   lilirudi: "Ninafanya kazi kupitia watu. Ninasubiri watu wangu wainuke na   kufanya kitu. "

Wewe na mimi   ni sehemu ya jeshi, mwili wa Kristo, na itachukua kila mtu kufanya sehemu   yake ya kubadilisha dunia hii. Mungu anataka kufanya kazi kupitia kwetu, na   Yeye anatuita sisi kuenenda katika upendo na kufanya kazi.

Katika 2   Wakorintho 8, Paulo alizungumza juu ya jinsi makanisa ya Makedonia yalitoa,   akisema

Tena walitenda hivi si kama   tulivyotumaini tu, bali kwanza walijitoa nafsi zao kwa Bwana; na kwetu pia,   kwa mapenzi ya Mungu.
Hiyo inashangaza sana, kwa   sababu hawakupeana fedha zao tu - walijitoa wenyewe. Mungu anatuita sisi   kuishi vivyo hivyo. Na mtu mmoja anayefanya kazi kwa Bwana ana uwezo wa   kufanya tofauti kubwa! Kwa hiyo utajitoaje kwa Bwana na kuwa wakala wake leo?

OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu,   ninakualika kufanya kazi kupitia mimi. Ninaamua kuweka ubinafsi na kuuchukua   upendo ili nipate kutumika na Wewe kubadili ulimwengu.

Andiko

siku 22siku 24

Kuhusu Mpango huu

Ahadi za kila siku ya maisha yako

Mungu ametupa ahadi tele ambazo tunahitaji kutembea ndani yake. Lakini ni muhimu kuzijua, kuziamini ili tuweze kuziona zikidhirika maishani mwetu. Kila siku, kuna ahadi kwa ajili yako. Unapoanza siku yako, pata kufahamu ahadi hizi! 

More

Tunataka kushukuru Joyce Meyer Ministries kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: tv.joycemeyer.org/kiswahili