Ahadi za kila siku ya maisha yakoMfano
Maisha Endelevu
Je! Unaishi maisha endelevu? Labda umepata mwenyewe kusema mambo kama, "Siwezi kufanya hivyo muda mrefu zaidi. Siwezi tu kuendelea hivi milele. " Unapokuwa na maoni kama haya, unasema ni nini, "Najua nina mipaka na kwamba nimefikia mwisho, lakini nitapuuza na kuona muda gani ninaweza kuendelea nayo."
Mwili wetu hutupa maonyo tunapoufanyiza kazi sana, kama uchungu hapa au maumivu huko. Lakini tunadhani, nitakuwa tu sawa, na tunapuuza maonyo mpaka tunakuwa wagonjwa sana hadi hatuwezi kupuuza.
Sijivunii jambo hili, lakini kwa miaka ishirini ya kwanza ya huduma yangu, nilifanya mengi sana wakati mwingi. Nilikimbia kwa madaktari na kujaribu kila aina ya dawa na vitamini. Madaktari walijaribu kuniambia kuwa nilikuwa nikijichosha sana, lakini niliwapuuza. Niliendelea kusukuma kufanya safari zote, kuzungumza kwenye kongamano, mikutano, na kadhalika- hadi nikajifadhaisha mwenyewe.
Hatimaye, nilitambua kwamba hatuwezi kupuuza mwongozo wa Mungu wa kuchukua wakati wa kupumzika bila kulipa gharama yake. Kwa hiyo nilifanya mabadiliko na sasa ninahisi vizuri zaidi kuliko nilivyokuwa.
Ikiwa unashikilia maisha yasiyoweza kudumu ,acha kukataa kufanya mabadiliko unayohitaji kufanya. Usisubiri mpaka kitu kitokee, kama kuharibika akili au tatizo la moyo. Fanya mabadiliko sasa ili uishi aina ya maisha Mungu anataka uishi.
Unapoishi njia ya Mungu, naweza kukuhakikishia kwamba utapata kugundua kiwango kipya cha amani katika maisha yako
OMBI LA KUANZA SIKU
Bwana, nionyeshe sehemu zisizoweza kudumu za maisha yangu. Ninaziwasilisha kwako. Niongoze katika mapumziko yako na amani leo, ili nipate kufurahia maisha yangu na kukutumikia kwa miaka ijayo.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Mungu ametupa ahadi tele ambazo tunahitaji kutembea ndani yake. Lakini ni muhimu kuzijua, kuziamini ili tuweze kuziona zikidhirika maishani mwetu. Kila siku, kuna ahadi kwa ajili yako. Unapoanza siku yako, pata kufahamu ahadi hizi!
More
Tunataka kushukuru Joyce Meyer Ministries kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: tv.joycemeyer.org/kiswahili