Ahadi za kila siku ya maisha yakoMfano
Wakati ni sawa kusema "hapana"
Katika Hesabu 11, Musa anatupa mfano wa kile tunaweza kufanya wakati tumesongwa na mambo mengi. Sema kuwa juu ya shinikizo - alikuwa akiwaongoza Waisraeli kupitia jangwa ile ilyofaa kuwa safari ya siku kumi na moja ambayo badala yake iliishia kuchukua miaka arobaini!
Watu walikuwa wamefadhaika na kulia juu ya hali yao. Katika mstari wa 14, Musa anamwambia Mungu, "Siwezi kubeba watu hawa peke yake, kwa sababu mzigo ni mzito sana kwangu."
Kama Musa, ni sawa kwa sisi kusema, "Nimefikia kikomo changu." Naam, Maandiko inasema, naweza kufanya yote kwa njia ya Kristo anayenitia nguvu(Wafilipi 4:13 ), lakini hiyo inazungumzia wakati ambapo sisi hukabiliana na majaribu mbalimbali na hali ambazo Mungu atatusaidia kupitia.
Haimaanishi kwamba tunapaswa kuchukua majukumu mengi sana thadi tulemewe kabisa, kama vile mwanamke anayelea watoto watano, anafanya kazi wakati wote, hutumikia kwenye bodi ya kanisa, na kadhalika.
Wakati mwingine, yote ni mengi sana ... na ni sawa kukubali hilo. Pia ni sawa kusema "hapana" kwa mambo fulani ili uweze kufurahia maisha kama vile Mungu alivyokusudia.
Hapa kuna habari: Wewe na mimi hatuna haja kuwa kama kila mtu mwingine au kuendelea na mtu mwingine yeyote. Mungu aliwaumba watu wengine kushughulikia kiasi kikubwa cha kazi, lakini watu wengine hawakuumbwa hivyo.
Kila mmoja wetu anahitaji kuwa kile ambacho Mungu alimuumba kuwa, na hatupaswi kuomba msamaha kwa hilo. Sisi sote tunahitaji kila mmoja kupata usawa wa wajibu Mungu ameweka kwa ajili yetu kuishi ndani ili tuweze kufurahia maisha yetu, badala ya kujifanya kuwa mgonjwa na msongo wa akili na shinikizo
Unapofikia kikomo chako, nenda kwa Mungu, kama Musa alivyofanya. Atakusaidia kupata afya mara dufu.
OMBI LA KUANZA SIKU
Mungu, wakati mwingine ni vigumu kwangu kupunguza mwendo na kusema "hapana" kwa jukumu zaidi. Nisaidie kuishi na usawa wa wajibu ulioumba kwa ajili yangu, hivyo nitaweza kuishi na amani yako na kufurahia maisha
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Mungu ametupa ahadi tele ambazo tunahitaji kutembea ndani yake. Lakini ni muhimu kuzijua, kuziamini ili tuweze kuziona zikidhirika maishani mwetu. Kila siku, kuna ahadi kwa ajili yako. Unapoanza siku yako, pata kufahamu ahadi hizi!
More
Tunataka kushukuru Joyce Meyer Ministries kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: tv.joycemeyer.org/kiswahili