Ahadi za kila siku ya maisha yakoMfano
Tuna uhuru wa kuendelea zaidi
Kumtafuta Mungu sio rahisi, lakini ina faida yake. Hata hivyo, huwezi kumfuatilia Mungu mpaka utakapoelewa uhuru wa kweli.
Mungu yuko katika biashara ya kutuweka huru, na ni jambo la ajabu kuwa huru kutoka hatia, hukumu, na daima kushangaa ni nini watu wanatuwazia.
Tunawekwa huru kutokana na wasiwasi wa kushindwa wakati tunajua sisi ni nani ndani ya Kristo. Hii inatuletea ujasiri wa kuwa na uwezo wa kusimama kidete na kutekeleza makusudi ya Mungu.
Mojawapo ya uhuru mkubwa Mungu alinipa ni uhuru wa kuwa mimi. Kwa miaka mingi nilijaribu kuwa kitu ambacho sikuwa, niliona ni kama nilihitajika kuwa kama hii au kama kile, ilhali wakati wote nilijua sikuwa kama kila mtu mwingine.
Hata hivyo, niliendelea kujaribu kuwa kama wengine mpaka nilipojifunza kupitia uhusiano wangu na Mungu ambaye aliniumba kuwa jinsi nilivyo. Hii pia imeniweka huru kutoka kwangu, hivyo nitaweza kumtazamia Yesu na kuwafikia wengine jinsi angependa.
Wafilipi 3 inasema Paulo alikuwa amedhamiria, kuwa hawezi kupungukiwa, kuwa na vitu ambavyo Kristo Yesu alikufa kwa ajili yake, kumjua Yeye na nguvu za ufufuo wake. Ninaamini wakati tunapozaliwa tena, kuna roho ya uamuzi ambayo inatokea ndani yetu.
Tunaweza kuiita shauku ya Roho Mtakatifu au bidii, na ndiyo inatupa msukumo tunaohitaji wakati wa magumu kusema, "Sitaacha kuwa na uhusiano wa karibu sana, wenye shauku, wa kina na kibinafsi na Mungu. Siwezi kuacha kuwa yote ambayo Kristo anataka mimi kuwa.
Uwe na shauku zaidi ya kukaa katika imani na kupokea ahadi za Mungu. Kumbuka, wewe ni wake na amekupa roho ya kutopungukiwa!
OMBI LA KUANZA SIKU
Mungu, nataka kuishi maisha mapya, bila kukoma kukutafuta Wewe na ahadi zako. Ninakuamini kunisaidie kuwa yote umeniumba kuwa na kupata uhuru wa kweli.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Mungu ametupa ahadi tele ambazo tunahitaji kutembea ndani yake. Lakini ni muhimu kuzijua, kuziamini ili tuweze kuziona zikidhirika maishani mwetu. Kila siku, kuna ahadi kwa ajili yako. Unapoanza siku yako, pata kufahamu ahadi hizi!
More
Tunataka kushukuru Joyce Meyer Ministries kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: tv.joycemeyer.org/kiswahili