Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ahadi za kila siku ya maisha yakoMfano

Ahadi za kila siku ya maisha yako

SIKU 14 YA 30

Kutupa hofu nje

Nataka kuzungumza na wewe juu ya neno la herufi nne: hofu! Wengi wetu tunaweza kukumbuka wakati tulipokuwa watoto, ikiwa tulisema neno baya, mama yetu alitishia kuosha mdomo wetu kwa sabuni. Naam, kama "hofu" ni neno chafu, herufi  nne, basi imani katika upendo wa Mungu ni sabuni!

Sizungumzi juu   ya imani hafifu. Ninazungumzia juu ya imani yenye nguvu katika upendo wa   Mungu usio na masharti, usio na ukomo, usioyumbayumba , na ulio kamilifu   kwetu.

1 Yohana 4:18 inatufundisha kwamba kuelewa upendo wa Mungu kwetu kutatuokoa kutokana na hofu zetu. Sasa hii haimaanishi kwamba hatuwezi kuhisi hofu, lakini imani katika Mungu na upendo wake itatusaidia "kufanya hivyo  huku tukiwa na hofu" kama tunapaswa.

 Mungu anataka ujue kwamba Yeye yu pamoja nawe. Yeye atakuongoza na kukuelekeza, ili uweze kuweka ujasiri na imani yako ndani yake! Kumbuka, upendo wake ni mkamilifu, hata wakati hatuko wakamilifu. Yeye hatatupenda zaidi au kidogo kwa sababu ya makosa yetu. Je, si ni vizuri kujua kwamba Mungu anakupenda katika hali uliyo ndani?? Je! Si wazo hilo linaweza kuimarisha imani yako na kupunguza hofu yako?

Wewe na mimi   tutahisi hofu mara kwa mara. Tunapofanya hivyo, tunaweza kumtazamia Mungu na   kujua kwamba atatuongoza kupitia hali yoyote tunayokabiliana nao. 

Ni upendo   mkamilifu wa Mungu-sio ukamilifu wetu-ambao hutoa hofu kila wakati.

OMBI LA KUANZA SIKU


Mungu, upendo wako pekee undio unaweza kuondoa hofu yangu, kwa hiyo nimeweka imani yangu ndani yako. Najua kuwa uwepo wako u pamoja nami na kwamba Wewe utaniongoza kupitia hali yoyote ya kutisha inayonikabili. Ninapokea upendo wako

siku 13siku 15

Kuhusu Mpango huu

Ahadi za kila siku ya maisha yako

Mungu ametupa ahadi tele ambazo tunahitaji kutembea ndani yake. Lakini ni muhimu kuzijua, kuziamini ili tuweze kuziona zikidhirika maishani mwetu. Kila siku, kuna ahadi kwa ajili yako. Unapoanza siku yako, pata kufahamu ahadi hizi! 

More

Tunataka kushukuru Joyce Meyer Ministries kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: tv.joycemeyer.org/kiswahili