Ahadi za kila siku ya maisha yakoMfano
Kuwa kinywa kwa Mungu!
Ikiwa unaweza kuelewa nguvu ya maneno unayosema, inaweza kubadilisha maisha yako! Kinywa chako ni chombo chenye nguvu, kwa Mungu au kwa adui. Kwa maneno mengine, unaweza kusema mazuri, kuimarisha, kusababisha mambo kuwepo katika maisha yako au kuzalisha mambo mabaya, yenye shida na ya kukata tamaa.
Sasa, siamini yeyote kati yetu anataka kuwa kinywa kwa shetani. Lakini ukweli ni kwamba, kinywa kinaweza kutumika kwa baraka au uharibifu, si tu katika maisha yetu, bali pia katika maisha ya wengine. Nimeiona katika maisha yangu mwenyewe. Kulikuwa na wakati ambapo kila kitu nilichosema kilikuwa hasi
Lakini Roho Mtakatifu alinifundisha jinsi ya kutumia nguvu za ubunifu za Neno la Mungu. Nilijifunza jinsi ya kuzungumza na milima badala ya kuzungumza juu ya milima katika maisha yangu. Ninachosema ni, nilijifunza kutumia ukweli wa Neno Lake kwa hali yangu, na baada ya muda, nilianza kuona matokeo mazuri na ya kudumu.
Kinywa ni kama kalamu na moyo wako ni kama kibao. Unaposema chochote mara kwa mara, huja kikawa ndani yako na kinakuwa wewe. Sio kitu unachojaribu kufanya tena, ni wewe mwenyewe.
Ningependa sana kuwa kinywa cha Mungu kuliko adui. Ninataka kusema ukweli wake na kufurahia maisha yangu.
1 Petero 3:10 inasema, Hebu anayetaka kufurahia maisha na kuona siku njema ... auzuie ulimi wake na uovu na midomo yake isiseme hila. Unataka kufurahia maisha? Basi kutumia mdomo wako kusema mambo ya Mungu katika maisha yako!
OMBI LA KUANZA SIKU
Bwana, najua kwamba kinywa changu ni chombo chenye nguvu ambacho kinaweza kutumika kwa Wewe au kwa adui. Ninawasilisha kinywa changu kwako. Nionyeshe jinsi ya kusema ukweli wako katika maisha yangu na katika maisha ya wengine.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Mungu ametupa ahadi tele ambazo tunahitaji kutembea ndani yake. Lakini ni muhimu kuzijua, kuziamini ili tuweze kuziona zikidhirika maishani mwetu. Kila siku, kuna ahadi kwa ajili yako. Unapoanza siku yako, pata kufahamu ahadi hizi!
More
Tunataka kushukuru Joyce Meyer Ministries kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: tv.joycemeyer.org/kiswahili